BREAKING NEWS

recent

WATU WAWILI WAFARIKI KWENYE MKUTANO WA MAGHUFULI MOROGORO

                           dr john pombe magufuli akiwa katika uwanja wa jamuhur morogoro

Watu wawili wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa kutokana na mkanyagano uliotokea juzi Uwanja wa Jamhuri, Morogoro katika mkutano wa kampeni za mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli.

jana Mwenyekiti wa CCM taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amewatembelea majeruhi hao waliolazwa Hospitali ya Mkoa Morogoro.

Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Ritha Lyamuya amesema walipokea watu 19 waliokuwa na majeraha yakiwemo ya kuvunjika maeneo mbalimbali ya mwili na kuongeza kuwa miongoni mwao, wawili walikufa kutokana na kuumia vibaya.

Aidha Dk Lyamuya alisema kuwa wagonjwa ambao bado wamelazwa wako 10 na wengine saba walitibiwa na kuruhusiwa.

Dk Lyamuya alisema kuwa waliokufa ni pamoja na mwanamke anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 42 na mtoto wa umri wa miaka 12 aliyejulikana kwa jina la Ramadhan Abdalah.

Uwanja wa Jamhuri juzi ulifurika watu wakati mgombea urais kwa tiketi ya CCM John Magufuli alipokwenda kwa ajili ya kufanya kampeni.

Mara tu baada ya Magufuli na viongozi wengine kuondoka uwanjani hapo, ndipo hali ya kusukumana na kukanyagana ilitokea getini wakati watu wakitoka.




WATU WAWILI WAFARIKI KWENYE MKUTANO WA MAGHUFULI MOROGORO Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com on 9/08/2015 10:22:00 AM Rating: 5
All Rights Reserved by habartz © 2014 - 2015
Designed by JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

HABARI NA MATUKIO YA KIJAMIII. Powered by Blogger.