SAMATTA AWASAFISHIA NJIA WATANZANIA
Mshambuliaji huyo pamoja na mwenzake Thomas Ulimwengu wamekuwa wakifanya vizuri kwenye klabu hiyo ambayo hivi karibuni ilitwaa Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika.
Dar es Salaam. Mafanikio ya mshambuliaji wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mbwana Samatta ni kama yamewafungulia njia wanasoka wa Kitanzania, ambao wana uhakika wa kupata nafasi ya kucheza soka la kulipwa nje ya nchi baada ya kufunguliwa milango ya kwenda huko.
Mshambuliaji huyo pamoja na mwenzake Thomas Ulimwengu wamekuwa wakifanya vizuri kwenye klabu hiyo ambayo hivi karibuni ilitwaa Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mbali na hilo Samatta alifanikiwa kuibuka mfungaji bora wa mashindano hayo huku pia akiwemo kwenye orodha ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora Afrika wa ndani.
Mafanikio ya Samatta yamewafungulia milango ya kucheza soka la kulipwa wachezaji wa Tanzania endapo wataongeza bidii.
Wakala anayemsimamia Samatta, Jamal Kisongo ametoa ahadi ya kuwauza nyota wa Kitanzania ambayo ikifanyiwa kazi vizuri na wanasoka hao wanaoshiriki Ligi Kuu nchini itawafanya wafikie anga za Samatta ama pengine kumzidi.
Wakala huyo ambaye pia anamsimamia mshambuliaji Haruna Chanongo na Hija Ugando aliyesajiliwa na Simba hivi karibuni, aliliambia gazeti hili kuwa atahakikisha kundi kubwa la wanasoka nchini wanakwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi, iwapo wataamua kwa dhati kufanya hivyo.
Kisongo alisema kuwa tatizo kubwa lililokuwa linawakabili wanasoka nchini ni kukosekana kwa mawakala wenye nia ya dhati ya kuwatafutia timu nje ya nchi, jambo ambalo kwa sasa halipo tena.
Alisema kuwa yeye binafsi amekuwa akihangaika usiku na mchana ili kutengeneza fursa kwa wanasoka nchini kupata nafasi ya kwenda nje na kucheza soka la kulipwa na anaamini kuwa hilo litatimia muda si mrefu.
SAMATTA AWASAFISHIA NJIA WATANZANIA
Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com
on
12/06/2015 12:26:00 PM
Rating: 5
No comments: