ZIFAHAMU NJIA KUMI (10) ZINAZOWEZA KUONGEZA UWEZO WAKO WA KUZAA MTOTO
KUPATA mtoto ni kitu
kinachofurahisha kwa wenzi, hasa waliofunga ndoa, ambao hawakubahatika kupata
mtoto wanakabili wakati mgumu sana. Baadhi ya wanawake hushika ujauzito mapema
tu baada ya kujamiana na wengine huchukua muda mrefu hadi kusababisha kukata
tamaa kwa wenzi hao.
Iwe unajaribu kupata
mtoto wako wa kwanza au wa sita (6), kuna njia nyepesi unazoweza kuzifuata ili
kuongeza uwezo wa kuzaa/kuzalisha. Zipo dondoo 10 za kukuwezesha
kuboresha uwezo wako wa kuzaa/kuzalisha, zipo kama ifuatavyo :-
(i) Dumisha uzito unaofaa
kiafya
Wanawake wengi
wanapenda kuwa na uzito wanaoupenda wao, ingawa sio kila uzito unafaa kwa kuwa
na hali nzuri ya uzazi. Kuwa na uzito kupita kiasi au kuwa na uzito mdogo
kupita kiasi kunaweza kusababisha ugumu katika kushika ujauzito. Uzito unaweza
kuathiri udhibiti wa homoni na hivyo kuathiri ovulesheni (yai kutolewa).
Kudumisha uzito unaofaa kiafya kunasaidia kudhibiti ovulesheni ya kawaida na kuongeza
uwezekano wa kushika mimba.
(ii) Weka mbegu za kiume katika Afya bora
Nini huanza kwanza,
mbegu za kiume au za kike? Wanawake wengi hutilia mkazo afya ya mayai, tarehe
za ovulesheni na idadi ya mayai, hata hivyo hupaswi kusahau umuhimu wa mbegu za
kiume. Idadi, harakati na umbo la mbegu za kiume ni sehemu muhimu ya afya ya
mbegu za kiume, lakini pia kuna vitu vinavyopaswa kufanywa au kutofanywa ili
kudhibiti afya bora ya mbegu za kiume.
Ili kuwa na mbegu
zenye afya, wanaume wanahamasishwa kudumisha uzito unaofaa kiafya, kula mlo
bora/kamili, kuzuia magonjwa ya ngono, kudhibiti mkazo(stress) na kufanya
mazoezi.
Kuepuka uvutaji wa
tumbaku, kudhibiti matumizi ya pombe, kuepuka sumu mbalimbali mfano sumu za
kuulia wadudu kwenye mbogamboga, hizi ni kati ya hatua zinazoweza kuchukuliwa
ili kukuza afya ya mbegu za kiume.
Ni vyema kuvaa nguo za
ndani zisizobana sana, tumia muda kidogo kukaa, kuepuka joto sehemu za siri
mfano kukaa kwenye jakuzi la maji moto, kuweka simu au kompyuta za kupakata
(laptops) karibu na korodani.
(iii) Jikinge na Magonjwa
Yanayoambukizwa kwa Kujamiana
Kujikinga na magonjwa
ya ngono hakutakulinda tu afya yako bali pia uzazi wako. Kisonono na Klamidia
(Chlamydia) ni kati ya magonjwa yanayoharibu uzazi kwa wanaume na wanawake.
Kuna njia zinazoweza kutumika kupunguza hatari ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa
mfano matumizi sahihi ya kondomu na kuwa mwaminifu kwa mpenzi wako.
(iv) Fanya tendo la Ndoa
Ikiwa mko katika
mahusiano ya kike na kiume na mnahitaji kupata mimba, fanyeni tendo la ndoa
mara nyingi iwezekanavyo hasa wakati wa siku nzuri kwa mwanamke kushika
ujauzito. Kwa wastani, siku nzuri za mwanamke kupata mimba kwenye mzunguko wa
hedhi huhusisha siku 5 kabla ya ovulesheni(yai kutolewa), siku ya ovulesheni na
siku 2-3 kufuatia ovulesheni.
Kufanya ngono kila
siku au kila baada ya siku mbili kutaongeza uwezekano wa kupata siku nzuri ya
kupata mimba tofauti na kufanya ngono mara chache.
(v) Zingatia ni mafuta
gani ya kulainisha utatumia
Baadhi ya wenzi
hutumia/huhitaji mafuta ya kulainisha wakati wa tendo la ndoa, lakini sio kila
mafuta yamefanyizwa kwa jinsi ile ile. Ikiwa utanunua mafuta hayo,
fikiria Pre-Seed, mafuta yaliyotengenezwa kulingana na ute wa seviksi
(mfuko wa uzazi).
Pre-Seed haina
Glycerin hivyo huruhusu mbegu kuogelea kwa uhuru kuelekea kwenye yai kwa ajili
ya urutubishwaji. Mafuta mengine kama Astroglide, KY Jelly na Touch huzuia
mbegu kusafiri vizuri.
(vi) Kunywa pombe kistarabu
Wanaume kwa wanawake
wanahitaji kuchukua tahadhari wanapochagua vinywaji ili kuongeza uwezekano wao
wa kuzaa/kuzalisha. Kwa wanaume, matumizi ya pombe kupita kiasi hupunguza
uzalishaji wa homoni ya testosteroni na kusababisha uume kutosimama sawasawa na
kuchangia kupungua kwa mbegu za kiume zinazotengenezwa. Kwa wanawake, matumizi
ya pombe kupita kiasi huweza kusababisha matatizo ya ovulesheni na hivyo
kuathiri uwezo wa kushika mimba.
(vii) Punguza matumizi
ya Kahawa
Kafeini inayopatikana
kwenye kahawa inaweza kuchangia kusababisha utasa ikiwa miligramu 500 au zaidi
hutumiwa na mtu, hii ni sawa na vikombe vitano vya kahawa kwa siku. Matatizo ya
kafeini yanayopendekezwa kwa siku ni miligramu 200-250.
(viii) Usivute Tumbaku/Sigara
Sote tunatambua
uvutaji wa sigara ni mbaya kwa afya zetu kiujumla, lakini unafahamu uvutaji wa
sigara unaweza kuathiri uwezo wako wa kupata mimba? Uvutaji wa sigara kwa
wanaume unaweza kusababisha uzalishaji mdogo na kasi ndogo ya mbegu za kiume na
uharibifu wa DNA wakati kwa wanawake husababisha kutokukomaa kwa ovari.
(ix) Acha mazoezi mazito
na kwa muda mrefu
Kufanya mazoezi ni
vizuri kwa afya yako kiujumla, ukiwa unajaribu kupata mimba mazoezi mazito
yanaweza kuwa hatari kwa hali yako ya uzazi. Mazoezi zaidi ya masaa 5 kwa wiki,
mazoezi magumu yanaweza kusababisha matatizo ya uzazi kwa sababu ya kukandamiza
ovulesheni na homoni ya projesteroni(homoni inayohusika na mzunguko wa hedhi
& utungwaji wa mimba). Ni vizuri kuzungumza au kumwona mtaalamu wa mazoezi
ili kuweza kukupangia aina na muda wa mazoezi utakao kufaa kulingana na
shughuli zako.
(x) Jihadhari na sumu
Kila mahali, kuna aina
fulani ya kemikali unazopaswa kujihadhari nazo kwa kuwa kemikali zingine
huchangia utasa kwa wanaume na wanawake. Wanaume na wanawake waliopatwa na sumu
za kuulia wadudu mfano kwenye bustani za mbogamboga, mbolea zenye sumu wanaweza
kupata matatizo ya uzazi.
Baadhi ya kazi kama kazi za viwandani,
kilimo, saluni na daktari meno wako katika hatari ya kupatwa na kemikali hatari
kwa afya yao ya uzazi.source dr mandai. tell. 0716 300 200/0784 300 300
ZIFAHAMU NJIA KUMI (10) ZINAZOWEZA KUONGEZA UWEZO WAKO WA KUZAA MTOTO
Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com
on
12/06/2015 09:11:00 AM
Rating:
No comments: