BREAKING NEWS

recent

JE UNAJUA SABABU YA KUCHOMOKA KWA CONDOMU AU KUPASUKA WAKATI WA TENDO LA NDOA


Kondomu ikipasuka wakati wa kufanya mapenzi, wahusika waliokuwa wanashiriki hukosa kinga dhidi ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa au VVU ikiwa mmoja wao anayo au kupata ujauzito.

Mambo Yanayochangia Kondomu Kupasuka

Kondomu hutengenezwa kwa ustadi sana ili ziwe imara na kuweza kuhimili mikiki yote wakati wa kufanya mapenzi. Kondomu zilizothibitishwa huwa hazipasuki kirahisi zinapotumika inavyopaswa. Hata hivyo mambo yanayochangia kondomu kupasuka;

· Kutumia kondomu iliyopitisha muda wake wa matumizi

· Kutumia kondomu ambayo haijahifadhiwa katika mazingira stahiki. Mfano kukaa eneo lenye joti kali au kukandamizwa sana.

· Kutumia vilainishi vyenye mafuta (oil based lubricants) huchangia kondomu kupasuka kirahisi. Tumia vilainishi vyenye maji.

· Kutoacha nafasi ya kukusanya shahawa sehemu ya mbele ya kondomu.

· Kutumia kondomu moja kwa zaidi ya goli moja

Kondomu inapopasuka kuna hatari ya kupata

· Magonjwa ya zinaa

· Viusi Vya UKIMWI (VVU)

· Ujauzito

Ikitokea kondomu imepasuka au imechomoka wakati unafanya mapenzi zingatia yafuatayo

· Acha kufanya mapenzi na toa uume kutoka kwenye uke kwa umakini.

· Tafuta kondomu ilipo, kama ipo kwenye uume ivue au kama imebakia kwenye uke basi itoe.

· Jioshe kwa maji safi kwenye uume au sehemu za nje za uke.

· Nenda chooni na ukojoe ili kondoa shahawa au majimaji ya uke kwenye njia ya mkojo

· Kama ulikuwa unafanya ngono ya mdomo; tema shahawa na kisha nawa mdomo kwa maji safi na uyateme. Usipige mswaki ndani ya masaa 3 baada ya kondomu kupasuka.

Kama mwanamke hakuwa kwenye njia yoyote ya kuzuia mimba basi anaweza kutumia vindonge vya dharura za kuzuia mimba(emergency contraception). Utatakiwa uanze kutumia dawa hizi ndani ya masaa 72 baada ya kondomu kupasuka au kuchomoka. Unaweza kupima mimba wiki 2 baada ya kondomu kupasuka.

Kujua kama ulipata maambukizi ya magonjwa ya zinaa unaweza kupima ndani ya wiki moja au mbili toka tukio litokee. Wakati mwingine dalili zinaweza kuanza kujitokeza mapema kabla ya kwenda kupima. Ikitokea hivyo basi hakikisha unaenda hospitali kwa ajili ya matibabu.

Ikiwa kondomu ilipasuka unakuwa kwenye hatari ya kuambukizwa endapo mwenzi wako ana VVU. 

Katika mazingira haya unaweza kwenda kupima kujua kama una maambukizi. Kama mwenzi wako imethibitishwa ana VVU na wewe hauna, unaweza pewa dawa za kuzuia virusi kuzaliana (ARV) na kupima tena kila baada ya mwezi mmoja kwa miezi 6 mfululizo. Maambukizi ya VVU hayaleti dalili ambazo ni rahisi kuzuiona au kutambua, hivyo usikae ukasubiri kuona dalili ili kujua kama umeambukizwa.

Kama imetokea kondomu ilipasuka, jitahidi kujifunza kwa umakini matumizi sahihi ya kondomu ili kuepusha jambo hili kujitokeza.
JE UNAJUA SABABU YA KUCHOMOKA KWA CONDOMU AU KUPASUKA WAKATI WA TENDO LA NDOA Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com on 2/02/2016 01:54:00 PM Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by habartz © 2014 - 2015
Designed by JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

HABARI NA MATUKIO YA KIJAMIII. Powered by Blogger.