JE UNAJUA JINSI YA KUZUIA MIMBA ???
Katika kipindi chote
cha maisha yake, mwanamke hutoa mayai ya uzazi zaidi ya 400. Hutoa yai moja kwa
kila mwezi kwa wastani wa miaka 30.
Yai hili linapokutana na mbegu ya kiume
wakati au baada ya kufanya ngono, linaweza kurutubishwa na mimba ikatungwa.
Ili
kuzuia mimba isitungwe, kuna njia za uzazi kuzuia mimba au zikijulikana pia
kama njia za uzazi wa mpango. Njia hizi za kuzuia mimba huzuia yai la mwanamke
kukutana na mbegu za kiume.
Katika kuchagua njia
ya kuzuia mimba ni muihimu kuzingatia;
·
Ufanisi wa ufanyaji
kazi wa njia hiyo.
·
Inafanya kazi kwa muda
gani (ukizingatia unataka kukaa bila kupata mimba kwa muda gani).
·
Madhara ya utumiaji wa
njia hiyo.
·
Kama inaweza kuachwa
na wewe kupata ujauzito mapema (kuna njia ambazo huchelewesha kidogo
kupata ujauzito baada ya kuziacha).
·
Kama itakulinda dhidi
ya magonjwa ya zinaa.
Kuna makundi ya aina
mbili ya njia za kuzuia mimba;
·
Njia za homoni
·
Njia zisizo za homoni
Njia za Homoni
Njia za homoni ni njia
ambazo zimekuwa zikitumika muda mrefu kuzuia mimba na zenye ufanisi mkubwa
sana. Hutumia homoni za kutengenezwa (progestin na oestrogen)
ambazo huzuia mayai ya kike yasitoke kwenye ovari.
Homoni hizi hufanana
na zile zinazotengenezwa mwilini. Ovari huendelea kutoa mayai pale ambapo
mwanamke anaacha kutumia njia hizi. Njia hizi huweza kuwa na homoni
ya progestin peke yake au mchanganyiko wa progestin na oestrogen.
Namna Zinavyofanya
Kazi
Homoni hizi hufanana
na zile zinazotengenezwa na mwili kwa kawaida. Huzuia mimba kwa kuongezeka
kwenye damu kwa kipindi tofauti na;
·
kuzuia ovari zisitoe
mayai ya uzazi.
·
kuufanya ute kwenye
shingo ya uzazi kuwa mzito na mgegu za kiume kushindwa kupita.
·
kuufanya mji wa uzazi
usiwe tayari kupokea kiinitete.
Njia hizi ni;
Vidonge Vya Kuzuia
Mimba
Hujulikana kama oral
contraceptives kwa kingereza na kuna vya aina mbili,
vyenye progestin na oestrogen (combined
oral contraceptive) na zenye progestin peke yake (progestin
only contraceptive).
Mwanamke hunywa
kidonge kimoja kila siku na vina ufanisi mkubwa katika kuzuia mimba.
Sindano za Kuzuia
Mimba.
Hujulikana kama injectable
contraceptives kwa kiingereza. Huwa zina homoni ya progestin ambayo
huchomwa kila baada ya wiki 12. Zina ufanisi mkubwa na hufanya kazi kwa muda
mrefu.
Vitanzi.
Vikijulikana kama
intrauterine contraceptive devices kwa kiingereza,
hupandikizwa kwenye mji wa uzazi na huwa na homoni yaprogestin. Hufanya
kazi kwa muda mrefu na kwa wastani wa miaka minne.
Vipandikizi
Vijiti huitwa implants kwa
kiingereza. Mara nyingi hupandikizwa kwenye mkono na huwa na homoni
ya progestin ambayo huingiapolepole kwenye damu kwa muda
mrefu.
Hufanya kazi kwa
wastani wa miaka 4, ingawa kuna vingine vikiwa na muda mrefu zaidi. Huweza
kutolewa pale mwanamke anapoamua.
Ufanisi
Njia hizi za homoni
zina ufanisi mkubwa, zikiwa na uwezo wa kuzuia ujauzito kwa zaidi ya asilimia
99.
Wanawake wasioshauriwa
kutumia njia za homoni;
·
Mwanamke mwenye
historia ya saratani ya matiti.
·
Mwanamke mwenye
shinikizo la damu la kupanda.
·
Mwanamke mwenye
ugonjwa wa moyo.
·
Mwanamke mwenye
matatizo ya damu kuganda kwenye mishipa (deep venous thrombosis).
·
Amefanyiwa upasuaji
ambao utasababisha asitembee kwa muda mrefu.
Faida ya Njia za
Homoni
Utumiaji wa njia za
homoni huwa na faida nyingi, hasa zifuatazo;
·
Hupunguza hatari ya
saratani za uzazi, ovari na utumbo.
·
Hupunguza maumivu ya
tumbo wakati wa hedhi.
·
Hupunguza kiasi cha
damu inayotoka wakati wa hedhi.
·
Ni rahisi kutumia na
zina ufanisi mkubwa.
Madhara ya Njia za
Homoni
Utumiaji wa njia hizi
huweza kuleta madhara pia, hasa zinapotumika kwa muda mrefu sana. Ingawa sio
lazima madhara yampate kila mtumiaji, madhara haya yanaweza kuwa;
·
Hatari ya kupata
saratani ya titi huongezeka.
·
Kulainika mifupa.
·
Damu kuganda kwenye
mishipa.
·
Kiharusi (stroke).
Njia Zisizo za Homoni
Njia hizi huzuia mbegu
za kiume zisikutane na yai la mwanamke. Zipo za aina mbalimbali, nyingine
zikihusisha upasuaji mdogo na mkubwa. Njia hizi hujumuisha;
Kondomu
Hii ni njia maarufu
sana, huzuia mbegu za kiume zisifikie yai la uzazi. Kuna kondomu za kike na
kiume, zote zikiweza kufanikisha hili.
Pia hukinga dhidi ya
VVU na magonjwa ya zinaa.
Njia za asili
Njia za kalenda, ute
wa kwenye uke na joto hutumika kuzitambua siku za hatari na hivyo kukwepa ngono
katika kipidi hicho. Pia kumwaga nje ni njia nyigine katika kundi hili.
Kufunga mirija ya
mayai (tubal ligation).
Upasuaji hufanyika na
mirija ya mayai hufungwa na kuzuia mbegu zisifikie mayai ya uzazi. Njia hii
ikitumika mwanamke hataweza kuzaa tena kwa kawaida.
Kufunga mirija ya
manii (vasectomy).
Upasuaji mdogo
hudfanyika na mirija ya kupitisha mbegu kutoka kwenye koroodani hufungwa. Hivyo
mwanaume hutoa shahawa zisizo na mbegu. Mirija ikifungwa mwanaume hawezi kuvaa
tena.
Vitanzi
Hivi hupandikizwa
ndani ya tumbo la uzazi, huwa vimetengezwa kwa kutumia madini ya shaba ambayo
huzuia mimba kutungwa .
Huweza kutumika mpaka
miaka 4. Tofauti na vitanzi vinavyotumika kwenye njia za homoni, vitanzi huwa
na madini ya shaba.
Njia hizi zisizo za
homoni zina ufanisi kwa viwango tofauti, kuna ambazo zina ufanisi mkubwa na
zile zenye ufanisi mdogo kama njia za asili. Kuna ambazo zinaweza kuleta
madhara na nyingine ambazo haziwezi kuleta madhara.
JE UNAJUA JINSI YA KUZUIA MIMBA ???
Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com
on
1/29/2016 02:19:00 PM
Rating:
No comments: