DIAMOND PLATNUMZ ASEMA KUMUOA ZARI HAKUTAMSHUSHA KIMUZIKI
mr&mrs Diamond
Platnumz
Diamond Platnumz amesema mpango wa kumuoa mpenzi wake Zari aliyezaa naye mtoto upo na haoni kama ndoa inaweza kumshusha kimuziki. Akiongea na EFM hivi karibuni, muimbaji huyo alisema haoni sababu yoyote ya kushindwa kumfanya Zari awe mke wake.
“Tufute imani fulani za vijana zinazowaambia kuwa ukiwa mwanamuziki ukioa unaweza ukayumba kimuziki. Shetta ana Shikorobo sasa hivi inahit sana na ameoa karibia ana miaka miwili,” alisema.
“Ni mipangilio yako mwenyewe, kuna wanamuziki wengi Ulaya ambao wanafanya vizuri na wameoa. Ni mipangilio yako mwenyewe na namna mnaweza kuishi vipi na mwenzako kuweza kuona mnawekaje mahusiano yenu na kulinda status mlizokuwa nazo,” aliongeza.
Zari na Diamond walijaaliwa kupata mtoto wa kike aitwaye Tiffah.
DIAMOND PLATNUMZ ASEMA KUMUOA ZARI HAKUTAMSHUSHA KIMUZIKI
Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com
on
9/08/2015 07:29:00 AM
Rating: