TFDA YATEKETEZA VIPODOZI NA BIDHAA ZILIZOISHA MUDA WA MATUMIZI
vipodozi feki na vilivyoisha muda wa matumizi
Mamlaka ya chakula na dawa TFDA kanda ya nyanda za juu kusini, imeteketeza vyakula na vinywaji vilivyopitwa na muda wa matumizi pamoja na vipodozi ambavyo vimepigwa marufuku kwa matumizi ya binadamu kwa vile vina kemikali zenye sumu,vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni kumi,vilivyokamatwa kwenye maduka mbalimbali katika manispaa ya sumbawanga mkoani Rukwa.
Mkaguzi wa Dawa wa mamlaka ya chakula na Dawa TFDA kanda ya nyanda za juu kusini Dakta Sylvester Mwidunda, akiongea wakati wa uteketezaji wa bidhaa hizo zenye madhara makubwa kwa matumizi ya binadamu,amesema msako huo ni endelevu kwa vile baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa sio waaminifu,na kwamba wamegundua kiwanda kidogo kinachotengeneza pipi bila ya kufuata taratibu na sheria, na kuweka anuani ya moshi kwa udanganyifu.
Naye afisa afya na usafi wa mazingira wa manispaa ya Sumbawanga Bw.sward Temba, amesema kuwa baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakikamatwa zaidi ya mara moja wakitenda kosa la kuuza vyakula ambavyo vimepitwa na tarehe zake za matumizi na pia vipodozi ambavyo vina sumu na vimepigwa marufuku,na kwamba sasa badala ya kuchangia gharama za uteketezaji wa bidhaa hizo, hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kufikishwa vyombo vya kisheria.
TFDA YATEKETEZA VIPODOZI NA BIDHAA ZILIZOISHA MUDA WA MATUMIZI
Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com
on
9/07/2015 07:23:00 PM
Rating: