UMOJA WA VIJANA GEITA WAZINDUA KITABU MAALUMU JE WAJUA KITABU GANI?
dr john pombe magufuli
Marafiki wa Magufuli Kanda ya Ziwa kupitia Umoja wa Vijana Mkoa wa Geita wamezindua kitabu maalum kiitwacho TINGATINGA ikiwa ni sehemu mojawapo ya kampeni ndani na nje ya mkoa huo kitakachomnadi mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dokta John Magufuli.
Vijana hao wamesema kitabu cha TINGATINGA kitasaidia wananchi kumjua kiundani Dokta Magufuli kwa kuwa kitasambazwa mijini na vijijini wakiwa na imani kuwa watakaosoma na kukielewa kitabu hicho watafanya maamuzi sahihi kwa mustakabali wa Taifa.
Vijana hao wamesema kwa uchunguzi wao wa awali waliofanya mjini na vijijini wamegundua wananchi wanamfahamu magufuli ila hawamjui kiundani na kuona njia pekee ni kuandaa kitabu maalum kinachomzungumzia Mheshmiwa Magufuli.
Baadhi ya waliohuduria uzinduzi huu wamesema kuwa ni jambo jema kwani kwa sasa kama si mjuaji wa siasa unaweza ukafanya maamuzi ya kishabiki.
Vitabu hivi vimeanza kugaiwa katika mitaa mbalimbali ya mjini ya Geita na maeneo mengine lengo likiwa kuwaeleza watanzania kiundani kuhusu historia ya Mgombea Urais kupitia CCM ambaye wamempa jina la tingatinga kutokana na umahiri wake wa kuchapa kazi bila hofu yoyote na hata kuleta maendelea ya haraka.
Hata hivyo vijana hao wamejipanga kutoa elimu kuanzia ngazi ya familia ili kila mwananchi awe na uelewa wa haki yake ya kuchagua kiongozi na wasifanye makosa ya kutokupiga kura Oktoba 25 licha ya kukabiliwa na changamoto ya kifedha kwa ajili ya kutoa kopi nyingi za vitabu ili ziwafikie wananchi..
UMOJA WA VIJANA GEITA WAZINDUA KITABU MAALUMU JE WAJUA KITABU GANI?
Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com
on
9/07/2015 12:50:00 PM
Rating: