KAMPUNI ZA SIMU 5 ZIPO MATATANI HAPA NCHINI TANZANIA KISA NI HIKI HAPA!
Dar es Salaam. Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA), imetoa adhabu ya faini ya Sh125 milioni
kwa kampuni tano za simu za mkononi kwa kushindwa kuweka mazingira
salama kwa wateja wao.
Kampuni hizo Airtel, Tigo, Smart, Halotel na Zantel, kila moja inatakiwa kulipa faini hiyo kabla ya Januari 29, mwakani.
Akitoa ufafanuzi wa adhabu hiyo jana, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk Ally Simba alisema imetolewa kwa sababu kampuni hizo zimeshindwa kutimiza matakwa ya Kanuni za Mawasiliano ya Kieletroniki na Posta ya mwaka 2011.
Sababu nyingine aliitaja kuwa ni kupuuza na kukaidi kufuata maagizo ya mamlaka iliyowapa Oktoba 16, mwaka huu kwa ajili ya kushughulikia matatizo hayo.
“Miezi miwili baadaye, tulifanya uchunguzi tukajiridhisha kuwa mitandao hiyo bado haikuwa salama kwa sababu watoa huduma walishindwa kufuata maelekezo yetu licha ya kuwapatia fursa ya kutoa utetezi wao,” alisema Dk Simba.
Alisema kushindwa kusimamia hayo, kumesababisha kuendelea kufanyika kwa vitendo vya utapeli wa kutumia ujumbe wa udanganyifu na ulaghai kwenye mitandao.
Dk Simba alisema jambo hilo husababisha watu kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu huku walaji (wateja) wakiumia.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura aliyefanya ziara katika ofisi hizo jana, aliwapongeza wafanyakazi wa TCRA kwa kazi nzuri wanayofanya.
Pia, alisema hatua hiyo iliyochukuliwa dhidi ya kampuni hizo ni matokeo ya kutotii sheria bila shuruti.
Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema wanayafanyia kazi maagizo hayo.
Wakati huohuo; Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Antony Mavunde ameziagiza kampuni za simu za Vodacom na Tigo kuwasilisha vibali vya kazi na makazi vya raia wa kigeni waliowaajiri leo.
Aidha, kampuni hizo zimetozwa faini ya Sh4 milioni kwa Tigo na Sh2.5 milioni kwa Vodacom baada ya kubainika kukiuka Sheria ya Usalama wa Mahali pa Kazi (Osha).
Mkurugenzi wa Tigo, Diego Gutierez alisema wafanyakazi wao wanayo mikataba, wanafuata sheria na kuahidi kufanyia kazi maagizo hayo yaliyotolewa.
Kwa upande wake, ofisa utumishi wa Vodacom, Comba Msomba alisema kampuni hiyo itafuata maelekezo waliyopewa na Serikali na kwamba baadhi ya vipengele walivifanyia kazi.

Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com
on
1/01/2016 08:40:00 AM
Rating:
No comments: