AFANDE SELE KUMALIZA KESI YA NENO ‘SIMBA’ KATI YA DIAMOND NA MR BLUE
’
Mfalme wa Rhymes, Afande Sele ameingilia kati malumbano kati ya Diamond Platnumz na Mr Blue juu ya umiliki halali wa jina ‘Simba.
Ikumbukwe kuwa Blue ndiye aliyelalamika kuhusu jina hilo lakini Diamond bado hajajibu kitu.
Afande anajipanga kurudia wimbo wake ‘Simba Dume’ ambao anataka awashirikishe Diamond na Mr Blue ili kila mmoja ajieleze yeye ni Simba wa aina gani! Patamu hapo…
Akizungumza katika kipindi cha XXL cha Clouds FM Jumanne hii, Afande alisema hatua hiyo itawafanya wasanii hao wajielezee wao ni simba wa aina gani.
“Jina la Simba nimeanza kulitumia toka mwaka 2000 katika albamu yangu ya kwanza, nilitoa wimbo unaitwa Simba Dume,” alisema.
“Nilimzungumzia Simba nikijifananisha na mimi. Sasa naamini kama kuna madogo wanagombania jina hilo ni vizuri kipindi hiki nikaandaa kolabo ya kuirudia nyimbo hiyo ili nifanye mimi, Blue na Diamond mwenyewe tukiwa kama Simba ili kila mtu ajielezee ni Simba wa aina gani kwa sababu mimi kwenye ile nyimbo nilijielezea mimi nafanana na Simba kwenye kila kitu mpaka tabia zangu,” aliongeza.
Afande anaamini hatua hiyo itasaidia kuitangaza nchi kwa sababu mnyama Simba ni mnyama anayepatikana kwa wingi nchini Tanzania.
Swali ni je ndoto ya Afande itatimia? Diamond atakubali? Blue atakubali?
Kama wakikubali, hii inaweza kuwa ni nafasi pekee kwa Afande kurejea tena kwenye chati.

Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com
on
12/29/2015 05:30:00 PM
Rating:
No comments: