BREAKING NEWS

recent

YAMOTOBAND NA KAYUMBA WAPO TAYARI KUKINUKISHA DAR LIVE

KAYUMBA (1)

MAMBO yameiva! Bendi funika bovu Bongo, Yamoto na Mshindi wa Bongo Star Search (BSS 2015), Kayumba Juma wanatarajia kukinukisha ile mbaya ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live, Mbagala- Zakhem jijini Dar, Desemba 19, mwaka huu.

YAMOTO-BAND-2

kizungumza na Ijumaa Wikienda, mratibu wa shoo hiyo, Mohamed Seif ‘Mudy K’ lisema kuwa mbali na kumtambulisha Kayumba atakayefanya shoo kwa mara ya kwanza siku hiyo, pia Yamoto wataachia ngoma yao mpya baada ya Cheza kwa Madoido ijulikanayo kama Imo.

“Kutakuwa na sapraizi kibao ambapo Baby J kutoka Zanzibar kwa mara ya kwanza atatambulisha wimbo mpya, familia yote ya Mkubwa na Wanawe itahamia Dar Live,” alisema Mudy K na kusisitiza kuwa kiingilio kitakuwa buku 10,000 tu.
YAMOTOBAND NA KAYUMBA WAPO TAYARI KUKINUKISHA DAR LIVE Reviewed by mudy mandai on 12/07/2015 09:26:00 AM Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by habartz © 2014 - 2015
Designed by JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

HABARI NA MATUKIO YA KIJAMIII. Powered by Blogger.