BREAKING NEWS

recent

EDWARD LOWASSA; IPO SIKU NITAINGIA IKULU KWA KURA ZA WATANZANIA


Aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kuungwa mkono Ukawa, Edward Lowassa amesema ipo siku ataingia katika Ikulu kwa kupigiwa kura na Watanzania.

Lowassa alitoa kauli mjini hapa jana katika Viwanja vya Shule ya Msingi Sinoni wakati akimuombea kura mgombea ubunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.

Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu matokeo ya urais yalipotangazwa na kumpa ushindi Dk. John Magufuli, Lowassa alisema anaamini kwamba Watanzania ambao kura zao ziliibwa ndiyo watakaompeleka Ikulu kwa vile bado yupo imara.

Alisema baada ya kutangazwa matokeo wapo baadhi ya viongozi na wafuasi wa Chama hicho waliomtaka atoe kauli kuhusiana na dhuluma aliyofanyiwa ya kuibiwa kura zake lakini aliwaambia hakuwa tayari kuingia Ikulu yenye mikono ya damu za Watanzania.

“Ni mara yangu kwanza kusimama mbele yenu tangu tulipomaliza uchaguzi mkuu. Naomba niwaambie nawapenda sana Watanzania sihitaji kuingia Ikulu kwa damu ya watu. Naamini Watanzania hawa hawa watanipeleka Ikulu siku moja, bado nipo imara.

“Hawa CCM na Serikali yao wamechakachua kura zetu, dunia inajua. Naomba niwahakikishieni tumeshinda Uchaguzi Mkuu, sisi ndiyo washindi hata wao wanajua. Tembeeni kifua mbele sisi ni washindi,” alisema Lowassa huku akishangiliwa kwa kauli mbiu za ‘Lowassa mabadiliko’, ‘Mabadiliko Lowassa’ na kuongeza:
EDWARD LOWASSA; IPO SIKU NITAINGIA IKULU KWA KURA ZA WATANZANIA Reviewed by mudy mandai on 12/10/2015 11:59:00 AM Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by habartz © 2014 - 2015
Designed by JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

HABARI NA MATUKIO YA KIJAMIII. Powered by Blogger.