AUNT EZEKIEL ASEMA ‘HAJAMCHAKACHUA MTOTO WA MOSE IYOBO,
Baada ya mashabiki katika mitandao ya kijamii kumshambulia kwa kuendelea kumficha sura mwanae Cookie, amejitokeza na kusema kwanini anafanya hivyo.
Akizungumza na tovuti ya Bongo 5, Aunt ambaye ana mahusiano na dancer wa Diamond Mose Iyobo amesema haoni sababu ya kumuonesha sura mwanae kwa wakati huu.
“Nitamuonesha mpaka nikiona walau amepata akaili kidogo”
“Kama angekuwa sio wa Mose kama anavyodai, baba yake asingemkubali, mwanangu amefanana kabisa na Mose. Wale wanaotaka kujua sura ya Cookie wachukue sura ya Mose alivyokuwa mtoto wataona wamefanana kila kitu, nimejikuta sihitaji tu kumuweka mwanangu katika media.” alisema.
AUNT EZEKIEL ASEMA ‘HAJAMCHAKACHUA MTOTO WA MOSE IYOBO,
Reviewed by mudy mandai
on
12/10/2015 11:55:00 AM
Rating:
No comments: