BREAKING NEWS

recent

BREAKING NEWZZZZZ; MTOTO ACHOMWA MOTO KWA KUTOANIAKA SHUKA ALILOKOJOLEA

Katika hali isiyokuwa ya kawaida Bi Kulwa Shasumuni mkazi wa Igunga Mkoani Tabora amemchoma moto mwanaye Hassani Faustino (9)kwenye mkono wa kushoto kwa kile alichodai ameshindwa kuanika shuka zake alizokojolea kitandani.

Wakizungumza kwa machungu kwa nyakati tofauti, baadhi ya majirani wamedai mama huyo amekuwa akimfanyia vitendo vya kikatili mwanaye mara nyingi hata wanapomzuia amekuwa akiwafokea na kuwaambia huyo si mtoto wao

Aidha, majirani hao wamedai walisikia kelele za mtoto Hassani “mama nakufa” na walipochungulia dirishani kwenye nyumba hiyo, walimwona mama huyo akiwa amemweka mtoto wake kwenye moto wa kuni na ndipo wao walilazimika kupiga kelele na hatimaye alimwachia.

Hata hivyo, majirani hao walibainisha kuwa mama huyo aliamua kumpeleka mtoto hospitali ya wilaya ambapo alilazwa wodi namba 8 kwa ajili ya matibabu kutokana na moto aliochomwa mkono wa kushoto.

Baada ya wiki mbili, mama huyo aliomba ruhusa hospitali ya kurudi nyumbani akidai atakuwa akimpeleka kusafisha kidonda jambo ambalo hakulitekeleza, badala yake alimfungia ndani kwa zaidi ya mwezi mpaka wananchi walipogundua na kutoa taarifa Ustawi wa Jamii waliofika kumchukua mtoto na kumrudisha hospitali.

Akizungumza akiwa katika Wodi Namba 8 katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga, Hassani alisema alikojoa kitandani kwa bahati mbaya na mama yake alipogundua, alimwamuru azianike shuka alizokojolea jambo alilosahau kufanya, ndipo mama yake alimkamata na kumtupia katika moto wa kuni uliokuwa ukiwaka kwa kasi.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Igunga, Abdallah Ombeni amesema hali ya mtoto huyo ni mbaya na wanajitahidi kuhakikisha wanamnusuru
BREAKING NEWZZZZZ; MTOTO ACHOMWA MOTO KWA KUTOANIAKA SHUKA ALILOKOJOLEA Reviewed by mudy mandai on 12/14/2015 07:44:00 PM Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by habartz © 2014 - 2015
Designed by JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

HABARI NA MATUKIO YA KIJAMIII. Powered by Blogger.