NEC YATANGAZA IDADI YA WABUNGE WA VITI MAALUM
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) leo imetangaza idadi ya wabunge wa viti maalumu ambao vyama vya vya siasa vya CCM, CHADEMA na CUF vimepata baada ya kupata angalau asilimia 5 ya kura zote halali za wabunge zilizopigwa siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 25, nchi nzima.
Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho kilipata jumla ya kura milioni 8.3 kimepata idadi ya wabunge wa viti maalum 64 wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambacho kilipata kura milioni 4.7 kimepata idadi ya wabunge wa viti maalum 36 na Chama cha Wananchi (CUF) kilichopata kura milioni 1.2, kimepata idadi ya wabunge wa viti maalum 10.
Aidha Jaji Lubuva ameanisha kuwa, jumla ya idadi ya wabunge wa viti maalum 113, wakati viti vitano vitatoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
NEC YATANGAZA IDADI YA WABUNGE WA VITI MAALUM
Reviewed by mudy mandai
on
11/06/2015 05:37:00 PM
Rating:
No comments: