WELBECK KUWA NJE MPAKA DISEMBA
Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Danny Welbeck atakuwa nje ya Uwanja mpaka mwezi Disemba baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye Goti .
Arsenal imeeleza kuwa matibabu kwenye Goti hilo hayakwenda vizuri na Wiki iliyopita ikaamuliwa afanyiwe operesheni.
Welbeck, aliumia Goti lake mwezi Aprili huku akiwa kaifungia timu yake ya Arsenal mabao 8 katika Mechi zake 34 tangu ahamie hapo kutoka Man United.
Hili ni pigo kubwa kwa Arsenal ambayo haikusajili mshambuliaji . Dirisha la usajili la kiangazi lilifungwa jumanne iliyopita.
Mfaransa Oliver Giroud anabaki kuwa mshambuliaji pekee wa kutumainiwa katika kikosi hicho.
WELBECK KUWA NJE MPAKA DISEMBA
Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com
on
9/04/2015 07:47:00 AM
Rating: