UKAWA KUUNDA TUME YA KUSHUGHULIKIA MIGOGORO SUGU NA INAYOUMIZA WANANCHI.
Mgombea urais wa vyama vinavyounda UKAWA Mh Edward Lowassa amesema akipata ridhaa ya wananchi ya kuwa rais wa awamu ya tano ataunda tume ya kushughulikia na kutoa haki kwa wananchi wakiwemo wa mkoa Katavi walioathiriwa na operesheni tokomeza na wanaoendelea kukumbwa na umaskini kutokana na migogoro ya ardhi.
Akizungumza na maelefu ya wananchi wa maeneo mbalimbali ya mkoa wa Katavi Mh Lowassa amesema asilimia ya wananchi wamekuwa wakiteseka kwa kutokana na viongozi wengi kutokuwa na uwezo wa maamuzi ama kutoa maamuzi yasiyo sahihi suala ambalo serikali atakayoiunda haitalifumbia macho hata kidogo.
Mwenyekiti wa Chadema Mh Freeman Mbowe amewataka watanzania kuungana na viongozi wanaotoka CCM kuhamia UKAWA kutokana viongozi wa CCM kukithiri kwa uonevu aliofanyiwa Mh Lowassa na viongozi wengine waliokuwa wanawania nafasi ya urais ambao walionekana hawafai.
Baadhi ya viongozi waliokiama chama cha mapinduzi akiwemo Hamisi Mngeja wamesema seraza UKAWA ni tofauti na zingine kwani zimelenga kuunda serikali ya wananchi na wala sio ya viongozi kama zinavyosema za vyama vingine.
Mgombea ubunge wajimbo la Mpanda Mh Jonas Kalinde na baadhi ya wananchi wamesema mabadiliko chini ya UKAWA yanadhihirisha kwa vitendo jinsi wananchi walivyochoshwa na serikali ya CCM ambayo imekuwa ya maneneo yasiyo na utekelezaji.
chanzo ITV
UKAWA KUUNDA TUME YA KUSHUGHULIKIA MIGOGORO SUGU NA INAYOUMIZA WANANCHI.
Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com
on
9/03/2015 08:03:00 PM
Rating: