BREAKING NEWS

recent

WANASHERIA NA WASOMI MBALI MBALI WATIA SHAKA UANASHERIA WA TINDU LISU



Wanasheria mbalimbali na wasomi kwa nyakati tofauti wamekuwa na mashaka na uwezo wa Tundu Lisu kisheria wakati akijibu hoja za Dr Slaa.

Wamekuwa wakiuliza na kushangaa Wakili Msomi mwenzetu alipokuwa anaongea na mwandishi wa habari wa VOA kwa njia ya simu. Tumeshangazwa na namna ambavyo alijibu maswali ya mwanahabari yule.

Anaposema kuwa Kamati Kuu ilishampitisha Dr Slaa tangu mwezi January na kurudia tena mwezi April, hapa anatoa tena kuwa kuna ubabaishaji wa demokrasia ndani ya CHADEMA kwa kukiukwa kwa katiba ya Chadema maana utaratibu wa kumpata mgombea haukufuatwa maana ilipaswa kuwe na uwazi kila mwanachama kugombea kwa kuchukua fomu kisha vikao husika vya chama kupitisha kwa kupiga kura.


Lakini pia anatupa maswali kama tangu mwezi January Slaa alipitishwa na Kamati Kuu, je ni kwanini mwezi July waliitisha mwanachama anayetaka kugombea achukue form ya urais ili hali tayari walikuwa na mgombea tayari?
Hapa wanakosa hoja ya Kusema Lowassa alionewa na mchakato wa kumpata rais ndani ya CCM maana nao walishafanya hayo mapema kama kweli mwenyekiti alifika kikao na majina yake mfukoni.

Pili anaposema kuwa mara baada ya kumpitisha Lowassa Dr Slaa alitupiwa vitu nje na mkewe maaana tatizo ni ufirst lady. Sasa hapa anatupa maswali ya kujiuliza kama Dr Slaa alifukuzwa na mkewe baada ya kunyimwa urais na huku kuna Picha walisambaza wakionyesha wazee wa baraza la wazee CHADEMA wakiwa nyumbani kwa Dr Slaa pamoja na mkewe na kueleza umma kuwa dokta amekubali kurudi kuongeza nguvu UKAWA na kusema kuwa alikuwa anapanga mikakati ya ushindi na kipindi hiko alikuwa likizo, je wazee wale walienda nyumbani kwa Dr Slaa kumwombea msamaha ili mkewe akubali kuendelea kuishi na Dr Slaa?

Kimsingi Lissu alipaswa kujibu hoja zilimtaja yeye na sio kuanza kuongelea privacy za watu, mbona yeye anayo mengi tu anayofanyiwa na mke wake hatusemi?

Kwa mfano Dr Slaa alisema kuwa kulikuwa na kikao cha watu wanne yaani Slaa, Mbowe, Lissu na Gwajima wakibishana kuhusu kama Lowassa ni Assets au Liability kwa CHADEMA?

Sasa Wakili Msomi Lissu alipaswa ama akubali au akanushe uwepo wa kikao hicho.

Na kama kilikuwepo na mazungumzo yalikokuwa yakizungumzwa ni tofauti na aliyosema Slaa atuambie ni mazungumzo yapi ni sahii.

Viongozi wa CHADEMA wakae na kutafakari namna bora ya kumjibu Dr Slaa na wafuasi wao wengi kwa hoja na sio majibu mepesi kwa hoja nzito na sio kutaka kuendelea kuwaburuza wafuasi wao.
WANASHERIA NA WASOMI MBALI MBALI WATIA SHAKA UANASHERIA WA TINDU LISU Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com on 9/05/2015 01:55:00 PM Rating: 5
All Rights Reserved by habartz © 2014 - 2015
Designed by JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

HABARI NA MATUKIO YA KIJAMIII. Powered by Blogger.