BREAKING NEWS

recent

HALI BADO TETE KWA CHAMA CHA UMOJA WA UKAWA


Siku chache mara baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Dokta Wilbroad Slaa Kujiuzulu na kuamua kuachana na siasa kutokana na kutokuridhishwa na utendaji ndani ya chama hicho baadhi ya vijana wamezidi kukihama chama hicho jambo ambalo linadaiwa kukidhoofisha chama hicho.

Baadhi ya vijana mjini Tabora waliokuwa wanachama wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya wananchi UKAWA wameandamana hadi ofisi ya CCM Wilaya na kudai wanajiunga na chama hicho baada ya kugundua kasoro za baadhi ya Viongozi wa Ukawa.

Wamesema wamegundua wamepotea baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA Dokta Wilbroad Slaa kuelezea mapungufu yaliyojitokeza katika kuwakaribisha na kuwapitisha wagombea mbalimbali wa chama hicho.

Vijana hao ambao wanadai kumuunga mkono Slaa wanadai kuguswa na maneno yaliyotolewa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA,Dk Wilbroad Slaa hivyo kuamua kukihama chama hicho.

Vijana hao mbali licha ya kuvihama vyama vyao,pia walichana kadi mbele ya ofisi ya Chama cha Mapinduzi,wakidai kuchoshwa na vyama vya upinzan
HALI BADO TETE KWA CHAMA CHA UMOJA WA UKAWA Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com on 9/05/2015 07:59:00 PM Rating: 5
All Rights Reserved by habartz © 2014 - 2015
Designed by JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

HABARI NA MATUKIO YA KIJAMIII. Powered by Blogger.