TANZANIA ITAENDELEA KUDUMISHA AMANI IWAPO KILA MWANANCHI ATAKEMEA CHUKI.
Tanzania itaendelea kudumisha amani na utulivu iwapo kila mwananchi atatimiza wajibu wake wa kukemea na kukomesha viashiria vya uvunjifu wa amani hususan uchochezi wa chuki.
Mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa vyombo vya habari nchini - MOAT Dr Reginald Mengi ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa kilele cha kongamano la amani, lililowashirikisha wadau mbalimbali.
Wakati wa kilele cha kongamano hilo washiriki walizindua tamko la pamoja lenye vipengere vitano kwa kurusha njiwa, kabla ya afisa mtendaji mkuu wa asasi ya Trinity Group East Africa Bw. Austin Makani kusoma tamko hilo.
Mapema katika mada yake kuhusu wajibu wa vyombo vya habari katika kudumisha amani na utulivu nchini, mwanahabari mwandamizi Dr Gideon Shoo alisema njia pekee ya kuirejesha nchi katika misingi bora ya uongozi ni kurejesha miiko na maadili ya uongozi wa umma, iliyofutwa kinyemela mwaka 1992 mjini Zanzibar.
TANZANIA ITAENDELEA KUDUMISHA AMANI IWAPO KILA MWANANCHI ATAKEMEA CHUKI.
Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com
on
9/18/2015 07:25:00 PM
Rating:
No comments: