MH EDWARD LOWASSA AMESEMA AKIINGIA MADARAKANI ATAPUNGUZA MSHAHARA WA RAIS
Mh Edward Lowassa
Mgombea urais kwa tiketi ya Ukawa Edward Lowassa ametangaza kuwa atapunguza mshahara wa rais endapo ataingia Ikulu.
Lowassa amesema haingii ikulu kutafuta fedha anaenda ikulu kwa kazi moja tu ya kuhakikisha wananchi wanakuwa na maendeleo. Amesema dhamira yake ni kuona taifa linasonga mbele kwa kasi ya ajabu.
Waziri mkuu huyo wa zamani amedai kuwa atapunguza mshahara wa Rais toka milioni 400 hadi milion 2 kwa mwezi!
Kwa upande mwingine Lowassa alidai kushangazwa na watu wanaosema anafuata fedha ikulu na kuwaambia kama mtu umeshindwa kutafuta fedha ujanani halafu utegemee upate fedha uzeeni hiyo ni ngumu kwa sababu uzeeni ni muda wa kusaidia jamii kwa kile ulichochuma ujanani.
Amesema wakati wa mabadiliko ni sasa, na mabadiliko hayo yatapatikana nje ya ccm kwani ipo haja ya kubadilisha mfumo hodhi wa chama tawala kama kweli tunataka kusonga mbele sisi kama taifa. Amesema yapo baadhi ya mambo Chama cha Mapinduzi hawawezi kuyabadilisha kwa kuhofia watu watafumbuka macho hivyo itatishia uhai wao.
MH EDWARD LOWASSA AMESEMA AKIINGIA MADARAKANI ATAPUNGUZA MSHAHARA WA RAIS
Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com
on
9/09/2015 09:04:00 AM
Rating: