HII NDIO IDADI KAMILI YA WANAFUNZI AMBAO WANAFANYA MTIHANI LEO NA KESHO
Mwanafunzi akifanya mtihani (picha kwa msaada wa mtandao) |
Ikiwa leo Septemba 09, 2015 wanafunzi wa darasa la saba wameanza mitihani yao ya kuhitimu elimu yao ya msingi inaelezwa kuwa jumla ya watahiniwa 775,729 watafanya mtihani huo leo hadi kesho utakaoshirikisha shule za msingi 16,096 nchini kote.
Kati ya watahiniwa hao, wavulana ni 361,502 sawa na asilimia 46.6 na wasichana ni 414, 227 sawa na asilimia 53.4.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde, alisema masomo yatakayotahiniwa ni matano ambayo ni Kiswahili, Kingereza, Sayansi, Hisabati na Maarifa ya Jamii.
“Mtihani wa kumaliza elimu ya msingi (PSLE) utafanyika leo na kesho katika shule 16,096 za msingi, huku watahiniwa waliondikishwa kufanya mtihani huo ni 775,729 kati yao wavulana 361,502 sawa na asilimia 46.6 na wasichana 414,227sawa na asilimia 53.4,” alisema.
Dk. Msonde alisema jumla ya watahiniwa 748,514 watafanya mtihani kwa Kiswahili na watahiniwa 27,215 watafanya wa Kiingereza ambazo ni lugha walizokuwa wakitumia katika kujifunza.
Alisema kati ya watainiwa hao, wasioona ni 76 wakiwamo wavulana 49 na wasichana 27 na watainiwa wenye uoni hafifu ambao huhitaji maandishi makubwa ni 698 kati yao wavulana ni 330 na wasichana 368.
Pia aliwataka wasimamizi wa mitihani kujiepusha na vitendo vya udanganyifu kwani Necta itachukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kukiuka taratibu za uendeshaji wa mitihani ya taifa.
Pamoja na hayo, kufuatia hali hiyo Baraza la Taifa la Mitihani limepiga marufuku wagombea wa vyama vya siasa kufanya kampeni karibu na maeneo la shule ili wanafunzi hao wafanye mitihani yao kwa utulivu.
HII NDIO IDADI KAMILI YA WANAFUNZI AMBAO WANAFANYA MTIHANI LEO NA KESHO
Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com
on
9/09/2015 03:29:00 PM
Rating: