MBASHA NA SIMULIZI YA KUTAKA KUJINYONGA
Emmanuel Mbasha.
KUMBUKUMBU ya kusikitisha! Siku chache baada ya kushinda kesi ya ubakaji wa shemejiye, Emmanuel Mbasha ameibuka na kusimulia jinsi alivyonusurika kujitoa uhai wakati kesi hiyo ilipokuwa ikiunguruma, Risasi Jumamosi linaandika.
‘Akimnong’oneza’ mwandishi wetu kwa njia ya simu Jumatano ya wiki iliyopita katika mahojiano maalum, Mbasha alisema kesi hiyo ilikuwa ikimuumiza moyo na kujiona hana thamani ya kuendelea kuishi hivyo njia bora ya kuepukana na kadhia hiyo ni kujitoa uhai.
Mbasha, ambaye alikuwa mume wa mwimbaji wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha alisema kitendo cha jamii kuaminishwa kuwa alitenda unyama huo, akiangalia heshima aliyonayo ikiwemo kueneza Injili kwa njia ya uimbaji, ilikuwa ni aibu mbaya ambayo kwa ujasiri wa kibinadamu haikuwa rahisi kukabiliana nayo.
Katika mazungumzo na mwandishi wetu, alisema mara nyingi watu wa karibu naye wakiwemo wazee wenye busara walishtukia njama zake za kutaka kujiua na kuamua kuwa naye karibu huku wakimpa nasaha za kumfariji na kwamba Mungu alikuwa akimpitisha kwenye jaribu hilo kwa makusudi maalum.
“Yaani wewe acha tu kaka, hakika nilitaka kujiua kabisa, ni bora ningesingiziwa mambo mengine na si kubaka, nikiangalia heshima yangu kwenye jamii, nikifikiria maisha ya jela tena kwa kosa la kusingiziwa, kwa kweli sikuona kabisa thamani yangu duniani,” alisema Mbasha.
TUJIKUMBUSHE
Mbasha alikuwa akikabiliwa na mashtaka mawili ya kumbaka shemeji yake mwenye umri wa miaka 17, kinyume cha sheria.Katika shitaka la kwanza, Mbasha alidaiwa kuwa Mei 23, 2014 alimbaka shemeji yake katika eneo la Tabata Kimanga huku katika kosa la pili la kesi hiyo, akidaiwa kufanya kosa hilohilo kwa mtu huyohuyo ndani ya gari.
Hukumu iliyomuacha huru ilitolewa Jumatatu ya wiki hii katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Ilala, ambapo hakimu Flora Mujaya alisema kwa mujibu wa sheria juu ya madai hayo, Mbasha hakuwa na hatia.
chanzo GLP
chanzo GLP
MBASHA NA SIMULIZI YA KUTAKA KUJINYONGA
Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com
on
9/26/2015 10:16:00 AM
Rating:
No comments: