DIAMOND, ZARI WAFANYA BONGE LA PATI!
Mwandishi wetu
Mastaa wawili wakubwa Afrika Mashariki, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ wanadaiwa kuangusha bonge la pati yenye kila aina ya viashiria vya ufuska, Risasi Jumamosi limeinyaka.
Chanzo chetu cha kuaminika ambacho kilikuwa miongoni mwa waalikwa kilichoomba hifadhi ya jina kilidai kuwa, siku hiyo ilikuwa ya kipekee kwa mastaa hao licha ya kwamba yaliyofanyika hayakuwa na sura nzuri mbele ya jamii.
Kwa mujibu wa mtoa taarifa huyo, awali, waalikwa wakiwemo mastaa kadhaa walianza ‘kupiga maji’ kwa staili ya taratibu au mdogomdogo hali iliyowafanya kadiri muda ulivyokuwa ukisonga, ndivyo walivyokuwa ‘wakipendeza’.
“Ilikuwa pati ya kufuru lakini watu walikuwa wachache na maalum, waalikwa walianza kwa kupata vinywaji mbalimbali na wale ambao ni watumiaji wa ‘maji machungu’ nao walipata chansi ya kujisevia walichotaka.
“Kwa kuwa pombe zilikuwa za kumwaga, watu walipombeka sana na ulipoingia usiku mnene, wengi walikuwa chicha,” kilidai chanzo hicho.
Ilidaiwa kuwa, wakati wengine wakiendelea kuburudika, baadhi walifikia hatua ya kusaula na kujirusha kwenye ‘swimming pool’ (bwawa la kuogelea) iliyopo nyumbani hapo na kuanza kuogelea na wakati mwingine kucheza muziki.
“Si unajua tena watu walikuwa nusu uhi, halafu baadhi walikuwa bwii, sasa unaweza kuvuta picha kilichokuwa kikiendelea kwenye maji, hata hivyo, ilikuwa full burudani aiseee,” kilitiririka chanzo hicho.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, mambo waliyokuwa wakifanya ndani ya mjengo huo hayakuwa ya kistaarabu kwani kubambiana ilikuwa sehemu ya shughuli hiyo.
“Lakini wapo baadhi ya wanaume ambao hawakuwa wastaraabu kwani walifanya vitendo ambavyo havikuwa vya kistaarabu tena kwa wanawake ambao siyo wao, ilikuwa na sura f’lani ya ufuska.
Chanzo hicho kiliendelea kunyetisha kwamba, pati hiyo iliyofanyika kwa siri huku mapaparazi wakinyimwa nafasi ya kushuhudia kilichokuwa kikiendelea ndani ya jumba la staa huyo ilihudhuriwa na baadhi ya mastaa wachache wakiwemo Shetta, Queen Darleen, TID, Young Dee, Romy Jones na wengine ambao walikuwa ni maalum.
DIAMOND, ZARI WAFANYA BONGE LA PATI!
Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com
on
9/26/2015 12:45:00 PM
Rating:
No comments: