BISHOP JOSEPHAT GWAJIMA AMEMJIBU DR SLAA LEO KATIKA HOTEL YA LAND MARK
Leo Jumanne Septemba 08, 2015 Askofu Gwajima anaongea na waandishi wa habari akitoa maelezo juu ya alichokisema Dk. Slaa wakati anaongea na waandishi wa habari pia kutoa maelezo ya uhusikaji wake kwenye tukio husika.
Gwajima: Mshenga ndio huwa anatumwa na mposaji, kwa hio siri zote za mposaji anazo mshenga lakini alikosea tu kwamba, mimi kusaidia kumleta mzee Lowassa CHADEMA ni kazi ya Mungu kwa sababu Biblia inasema heri wapatanishi maana hao wataitwa wana wa Mungu. Kwa hio, kwa desturi wanasiasa huwa hawaelewani mpaka wapate mtu wa kuwaleta pamoja kwa sababu wanasiasa wanageukana muda wowote.
Kwa sababu hio mimi nilisimama pale sio kwa sababu ni bora kuliko wengine lakini kwa sababu nilikuwa mtu sahihi kwa wakati ule kuwaleta pamoja hawa wanasiasa wawili na wengine ili kusudi tukomboe taifa letu kama ilivyokuwa kiu ya Dk. Slaa. Kwa hio nikawakutanisha pamoja, nilianza na Dk. Slaa mwenyewe mpaka ikafika sasa Slaa mwenyewe akaniita twende tukamwone mwenyekiti, tukaonana na mwenyekiti kukawa na mazungumzo ya muda mrefu baadae wakakubaliana vizuri.
Mpaka tarehe 26/07/2015 siku ambayo mheshimiwa Edward Lowassa alikuwa anaingia CHADEMA, kulikuwa na mkutano uliofanyika pale bahari beach hotel, kwa hio usiku ule Mheshimiwa Lowassa alikuwa anakuja kuingia CHADEMA kwa maana ya kuonana na kamati kuu ya CHADEMA. Na kwa sababu mimi namediate niko katikati, ni vizuri niwepo ili nihakikishe mheshimiwa Edward Lowassa ameingia CHADEMA kwa usahihi, hajaonewa na hajamuonea Dk. Slaa.
Tulikwenda mpaka kamati kuu ya CHADEMA, nataka niongee kwenye platform ya mtumishi wa Mungu kwa sababu wanasiasa wanaweza kudanganya lakini mimi nilikwenda mpaka nikawaomba watu wa CHADEMA, mimi si mmoja ya kamati kuu ya CHADEMA, nawaomba mniruhusu niingie kamati kuu ili nihakikishe mheshimiwa Edward Lowassa amefika salama.
Na hili jambo ni la kawaida, mtu anaweza kusema ulikuwa mchungaji ulifanyaje hivyo! Siku zote wanaogombea Urais, siasa, vyeo, nafasi, power, ukurugenzi wanaanzia kwa waganga wa kienyeji, wanazindikwa, wanachanjwa chale. Ni jambo zuri kama mtu ameanzia kwenye nyumba za ibada. Na mtu hatakiwi aone jambo hili ni baya, ni zuri kuliko yote badala ya kuanzia kwa waganga wa kienyeji, ameanzia kwenye nyumba ya ibada.
Usiku ule mheshimiwa Lowassa, sasa akaingia kwenye kamati kuu na mimi nilikuwemo ndani ya kamati kuubkuhakikisha amefika salama na alipokelewa pale nje na Dr Slaa na Prof Baregu na mwenyekiti wa chama na watu wengine. Mzee Lowassa akaongea, wote wakasimama kwa pamoja wakapiga makofi, wakamkubali, wakampokea. Mkutano ukamalizika usiku kama saa sita hivi, basi nikafurahi mimi nimeimaliza kazi ya kuwa mpatanishi kwa watu ambao kwa nature ya kawaida wasingeelewana.
(Gwajima anaonyesha meseji aliyotumiwa na Dr. Slaa kuhusu kustaafu kwake siasa)
Gwajima: Kama Dr. Slaa anakuja aje atoke hapa akane aone mambo ya mshenga yalivyo, watu wanashangaa Slaa anaweza kufanya haya! Si yeye ni mama. Slaa alikuwa adili, sasa uzoefu wa ndoa hana, bora sisi wachungaji tunaoa.
Nilimpa maneno ya matumaini, nitamtafuta mkewe niongee nae, nilimtafuta mkewe rose garden. Nilianza mimi kumbembeleza amruhusu baba aendelee na hayo maelezo nimeyarokodi na mimi ni mtu wa kurekodi. Alisema ameshawaambia watu yeye atakuwa first lady, siku iliyofata tarehe 28, nilimuita yule mama Kibo complex.
Tukakaa ndani ya gari yake, nilikuwa mimi na mtu mwingine, niliendelea kurekodi tena. Ilikuwa ni siku Lowassa anapokea kadi bahari beach, nawaonyesha hio sio kwa mumuone Slaa mbaya. Saa nane mchana akasema nimekubali Slaa arudi aingie kazini kwa sharti mkutano wa kumpokea Lowassa ufutwe. Nikamwambia hilo halitatokea milele.
Watu wengi sana wametumwa kuongea na yule mama, akiwemo mzee Ndesamburo ambae alishindwa kumpata yule mama, kumbe yule mama anaongea kwa karibu sana na mchungaji Max hivyo akampeleka Ndesa.
Mchungaji Max: Ilifika mahali chama kiliacha majukumu yote kumpata yule mama kuongea na Ndesamburo, yule mama alisema CHADEMA wanacheza mpaka waongee nami, alisema CHADEMA ni waongo na wanafiki, kwanini watufanya mpaka tumekosa urais. Mpaka juzi nilikuwa nawasiliane nae lakini maongezi yake kwa ujumla anasema kwanini wameachwa kugombea Urais, kwa jinsi alivyokuwa anaongea nikajua hata Dokta hawezi kuchomoka.
Slaa alisema Josephine amemfungia Serena, ukweli mimi naufahamu, ishu ipo kwa mkewe, Dr tumeshampoteza.
Gwajima: Siku moja nilikuwa Korea, Slaa alisema mkewe amedondoka amezimia, nikaomba kwenye simu mkewe akaanza kupiga kelele, nilimwambia Dr. Slaa sijawahi kuona mambo haya. Nilikuwa namsindikiza mke wangu kwenda London, cha kushangaza nikamkuta mke wa Dr Slaa airpot amekuja kusindikiza, umeambiwa na nani! Akasema nimejisikia tu! Baada ya check in, kurudi mke wa Dr. Slaa alidondoka chini, mashetani yalikuwa yanamrudia.
Siku nyingine Slaa alinipigia simu mkewe amedondoka, haya ni mashetani, Slaa anaongozwa na mwanamke wa aina hii. Ikulu pangekalika? Slaa si yeye, kuna tatizo limetokea.
Slaa Serena alisema kwenye mkutano wa CHADEMA watu waliletwa na malori na mabasi, mlioenda mjiulize ni kweli? Mtu anaesema uongo wa mchana, anasema Gwajima anasema maaskofu wa katoliki wamepewa hela. Kanisa katoliki ndio kanisa credible sana duniani.
Kwanini Slaa amesema! Kwanza kuwaondolea credibility, maaskofu hawa wamemsomesha, leo maaskofu 30 anawasingizia. Kwa mtu unaemuamini Slaa unaweza kusema anasema kweli lakini nimekuonyesha mazingira kwanini!
Anatukana maaskofu wa protestant na katoliki, nani aliemtuma! Slaa aliulizwa unalindwa na usalama wa taifa? Alisema kweli, watu wa usalama wanambeba kwenda Serena, Azam na Star Tv kutukana maaskofu. Maaskofu hawaruhusiwi kujihusisha na siasa lakini ni wapiga kura, Je, atakupa kura! Je waumini wao watakupa kura! Strategy hii imeshindikana wafikirie nyingine. Bahati mbaya hii ilikuwa silaha yao ya mwisho.
Mababa askofu wa kanisa katoliki hawakupewa rushwa wala mimi sijapewa rushwa, anasema nilikuwa nazunguka kwenye ndege na Lowassa. Mimi nina ndege yangu na siombi kibali kuzungumza mtu.
Usalama wa taifa sio wa CCM, mnatafasiriwa nyie ndio mnatukana maaskofu, usalama wa taifa mnamuharibia Magufuli, mwacheni aendelee kampeni zake kwa amani.
Siku nitakayorudi kumjibu Slaa akinisemesha, nitasema Slaa alivyokutana na watu wa usalama wa taifa Afrika kusini. Usalama mtapomuongoza tena huyo mtu wenu wenu atukane maaskofu, nitawalipua na bomu na macho yenu hamtafungua tena
Uadalifu wa Slaa
Gwajima: Alisema baba askofu lazima mtubu, najiuliza yeye ni msafi kuliko sisi? Slaa aliacha wito ambalo ni tatizo tayari, zaidi ya kuacha wito ukaoa! Nikija tena nitaleta watoto aliowazaa na uhusiano wa yeye kutoka. Ukaa na mke na watoto ukatelekeza, haitoshi ukaenda kuoa mke wa mtu mwingine. Kamili akaweka zuio mahakamani.
Slaa alisema Ridhwani nauza madawa ya kulevya, leo Slaa ndio anao aliowasema, anaemuongoza Slaa akome na akome kabisa. Watu wa usalama kazi yenu ni kulinda nchi iwe na amani na sio kuichafua.
Kinachosumbua ni wakati na majira, 20 kabla ya kristo kulikuwa ana mtu aliehubiri ubudha, akaijaza Ubudha kwa sababu yalikuwa majira yake. Baada ya hapo, karne ya kwanza alitokea Yesu kristo na kukutana na upinzani wa ajabu, ukifika wakati waksema wamemkamata.
Kweli ukiizika ina tabia ya kufufuka na ukiizika haiwezi kufa tena, akaja kutokea Mtume Muhammad japo alipata upinzani mkubwa leo Uislam umeenea sana. Nami niseme mfate majira, msishindane nayo. Tanzania ni kubwa kuliko watanzania.
BISHOP JOSEPHAT GWAJIMA AMEMJIBU DR SLAA LEO KATIKA HOTEL YA LAND MARK
Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com
on
9/08/2015 09:10:00 PM
Rating: