BREAKING NEWS

recent

DC-KITETO AKABIDHI HATI ZA KIMILA KWA WAFUGAJI

DC-KITETO AKABIDHI HATI ZA KIMILA KWA WAFUGAJI

Wankyo Gati, Kiteto


Add caption

Mkuu wa wilaya ya Kiteto, mkoani wa Manyara, Tumaini Magesa amewataka wafugaji na wakulima katika vijiji vitatu vya vya Kimbo, llole na Napalai vinavyounda ushirika wao wa kutunza ardhi kwa ajili ya malisho ya Mifugo unaofahamika kama OLENGAPA kuheshimu taratibu za hati miliki za kimila na usajili wa ushirika huo kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.
Ametoa rai hiyo katika kijiji cha ENGANG’ONGARE alipokuwa akikabidhi hati miliki tisa za kimila na vyeti vitatu vya usajili wa Ushirika wa wafugaji wa kuendeleza nyanda za Malisho, uliopo katika mpango wa kimataifa wa kuendeleza maeneo yaliyohifadhiwa kwa kutumia taratibu za kiasili au kimila na kutekelezwa na Jumuiko la Mali Asili Tanzania (TNRF) na KINNAPA.
Ushirikiano huo ni baina ya ushirika huo, wizara ya mifugo na halmashauri hiyo chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa(UNDP)na Umoja wa Ulaya (EU).
Bwana Magesa amesema ni vizuri kila eneo matumizi yake yawe yamepangwa na kujulikana kisheria; ili kuondoa changamoto ya migogoro ya ardhi, iliyokuwa ikijitokeza wilayani humo, miaka iliyopita na pia kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.
Baadhi ya wenyeviti wa vijiji hivyo pamoja na akina mama wa jamii ya kifugaji wamefurahia mpango huo na kusema kwamba utakuwa chachu kubwa ya kupiga hatua ya maendeleo, pamoja na kumaliza kabisa changamoto ya migogoro ya ardhi iliyokuwa ikijitokeza baina ya wafugaji na wakulima.

DC-KITETO AKABIDHI HATI ZA KIMILA KWA WAFUGAJI Reviewed by Geahtv on 6/30/2020 01:55:00 PM Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by habartz © 2014 - 2015
Designed by JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

HABARI NA MATUKIO YA KIJAMIII. Powered by Blogger.