VYAKULA MUHIMU KWA MAMA ANAYETARAJIA KUPATA UJAUZITO
Ishu ya kupata mtoto ndani ya familia ni moja ya mambo muhimu ambayo ndoa nyingi huhitaji na hufurahia sana pale hali inapokuwa hivyo.
Sasa shida huwa inakuja pale endapo wanandoa wanapokaa ndani ya ndoa kwa miaka kadhaa wakitafuta mtoto/ watoto lakini wasifanikiwe hapo ndipo tatizo huanza yakiwemo maneno ya kejeli na hata kufikia hatua za kutalakiana pia.
Kutokana na kutambua thamani ya mtoto kwenye ndoa leo nimeona nikufahamishe hivi vyakula vichache ambavyo vikitumika hurahisisha zoezi zima la upatikanaji wa ujauzito.
Pia mayai yana kirutubisho kiitwacho antioxidants na carotenoids ambavyo kwa ujumla wake husaidia sana kuongeza uwezekano wa mwanamke kushika ujauzito.
Hii ni moja ya aina ya mbogamboga ambayo husifika kwa kuwa na vitamin C yakutosha na kwa mujibu wa utafiti uliowahi kuchapishwa kwenye jarida la Fertility and Sterility waliainisha kuwa kiasi kingi cha vitamin C ni moja ya vitu muhimu sana kwa wanawake wanaohitaji kushika mimba.
Kwa upande wa wanaume inaelezwa kuwa vitamin C husaidia kuimarisha ubora wa mbegu za kiume 'sperm' lakini pia vile vile huwasaidia kina mama kuepukana na matatizo ya kuharibika kwa mimba mara kwa mara.
Pia broccol ina utajiri mkubwa wa vitamin B, madini ya calcium, chuma na zinc ambapo vyote kwa pamoja ni muhimu kwa mama anayehitaji kushika ujauzito.
Ulaji wa samaki nao ni muhimu kwani ndani ya samaki kuna kitu kiitwacho 'Omega 3' ambayo kwa kiasi kikubwa hurekebisha homoni za mwanamke na husaidia pia kupunguza msongo wa mawazo ' stress'
Hayo ndiyo machache kuhusu vyakula ambavyo vinauwezo wa kuongeza uwezekano wa kushika ujauzito kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com
VYAKULA MUHIMU KWA MAMA ANAYETARAJIA KUPATA UJAUZITO
Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com
on
1/13/2016 11:12:00 PM
Rating:
No comments: