BREAKING NEWS

recent

OKWI AIINGIZA MATATANI SIMBA

Aliyekuwa mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi.

SIKU chache baada ya gazeti hili kuripoti kuwa aliyekuwa mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi yupo tayari kurejea klabuni hapo endapo itatimiza masharti yake pamoja na yale ya timu yake ya Sonderjyske ya nchini Denmark, kuna uwezekano mkubwa Simba ikaingia matatani kwa ajili ya kutaka kufanikisha zoezi hilo.

Sonderjyske imeitaka Simba itoe dola 120, 000 (zaidi ya Sh milioni 250) ilizozitoa wakati inamsajili ili iweze kumruhusu Okwi kurejea klabuni hapo kutokana na kutokuwa na mpango naye kwa sasa.

Mbali na sharti hilo la Sonderjyske, Okwi pia ametoa yake akiitaka Simba impatie mshahara wa dola 5,000 (zaidi ya Sh milioni 10 kwa mwezi) na dola 30,000 (zaidi ya Sh milioni 60) ili aweze kutua klabuni hapo na kuifanya kazi yake kama wengi wanavyomfahamu.

Kutokana na hali hiyo, uongozi wa Simba hivi sasa unahaha kutafuta fedha hizo ili uweze kumrudisha nyota huyo ambaye amekuwa na bahati nzuri na klabu hiyo.

“Hii tunaiona kama ni bahati kwetu lakini tatizo tulilonalo hivi sasa ni fedha, klabu yetu haina fedha hizo ambazo jamaa hao wanazitaka lakini pia mshahara ambao Okwi anataka pamoja na ada yake ya uhamisho anayotaka ni kubwa kwetu.

“Tunachofanya hivi sasa ni kutafuta watu ambao wanaweza kutusaidia katika hilo kama itawezekana tuweze kumsajili kabla ya dirisha hili dogo la usajili kufungwa Desemba 15, mwaka huu, kama itashindikana basi itatubidi tuachane naye asije kutuingiza matatani,” kilisema chanzo hicho cha habari.

Alipoulizwa kuhusiana na suala hilo, Rais wa Simba, Evans Aveva, alisema: “Sina taarifa yoyote kuhusiana na Okwi, ila kama unavyojua Simba ni taasisi kubwa inawezekana jambo hilo lipo.”
OKWI AIINGIZA MATATANI SIMBA Reviewed by mudy mandai on 12/11/2015 01:41:00 PM Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by habartz © 2014 - 2015
Designed by JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

HABARI NA MATUKIO YA KIJAMIII. Powered by Blogger.