BREAKING NEWS

recent

MAKUNDI MATATU YA UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO NA DALILI ZAKE

KUNA makundi matatu makuu ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo na leo tutajadili kwa kina aina hizo za magonjwa haya ya tumbo kama ifuatavyo:

1. Gastric Ulcers: Aina hii ya vidonda vya tumbo hutokea kwenye mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo.

Vidonda hivi hutokea katika utumbo kwa sababu mbalimbali kama vile mtu kupata maambukizi ya bakteria aina ya Helicobacter pylori.

Imegundulika kuwa zaidi ya asilimia 50 ya watu duniani wana vimelea hivi katika utumbo na huwa ni vigumu kuonesha dalili yoyote ya kuugua maradhi haya.

Aina hii ya vimelea vya bakteria husababisha karibu asilimia 60 ya vidonda vinavyotokea kwenye tumbo na huitwa kitaalam Gastric Ulcers.

2. Duodenal Ulcers: Aina hii huwapata watu kutokana na kushindwa kwa mfumo wa kinga mwilini ambao huua na kuondoa kabisa vimelea vya kinga ndani ya mwili.

Matokeo ya kushindikana huko kunasababisha kuwepo kwa uambukizi wa kudumu katika kuta za tumbo ambao kitaalam huitwa Chronic Active Gastritis, hivyo kuharibu mfumo na uwezo wa kuta za tumbo kutunza homoni ya Gastrin ambayo kazi yake ni kuhakikisha tumbo linakuwa na tindikali (acid) inayotakiwa tumboni.

Acid hii iitwayo Gastric Acid, ikizalishwa kwa wingi tumboni husababisha kuchubuka kwa ukuta wa tumbo na mtu huyo kuambiwa ana vidonda vya tumbo.

Lakini ukuta wa utumbo hujilinda na madhara yatokanayo na tindikali ya utumbo yaani Gastric Acid kwa kuwa na utando laini (mucus) ambao hutolewa na vichocheo vijulikavyo kama Prostaglandins.

Hata hivyo, kuna dawa ambazo huharibu mfumo wa kutengeza vichocheo hivi yaani Prostaglandins na hivyo kufanya kuta za tumbo kukosa mucus za kuzilinda na mashambulizi ya tindikali, hali ambayo hufanya vidonda vya tumbo kuibuka.

3. Ulcers in small intestine:
Kundi hili ni wale wagonjwa wanaougua ugonjwa wa vidonda kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo yaani Small Intestine na maumivu yao makali husikia wanapokuwa na njaa na hupata nafuu pindi anapokula.

DALILI ZA MARADHI HAYA
Dalili kubwa ni mgonjwa kusikia maumivu makali au kiungulia maeneo ya chembe ya moyo ambayo kitaalam huitwa Epigastic Pains.

Wengine maumivu hayo huwatokea wakati wa kula chakula au mara tu baada ya kumaliza mlo wao. Hii ni kwa wale wenye vidonda vya tumbo vinavyojulikana kama Gastric Ulcers.

Dalili nyingine ya maradhi haya ni wagonjwa kuvimbiwa au tumbo kujaa gesi, kucheua au kutoa hewa chafu mara kwa mara.

Wengine huongezeka mate yanayoshuka tumboni baada ya kucheua au kusikia kichefuchefu na kutapika na kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito.

Hali ikiwa mbaya mgonjwa hutapika damu au kupata haja kubwa ya rangi nyeusi au kahawia au kilichochanganyika na damu.

Wenye vidonda vya tumbo wakitumia dawa za kupunguza maumivu bila kufuata ushauri wa daktari watakuwa wanapata kiungulia cha muda mrefu, kucheua na kutapika baada ya kula chakula.
TIBA

Makundi yote hayo ya ugonjwa wa tumbo hutibika. Daktari akigundua mgonjwa ana matatizo haya atatumia dawa mbalimbali za antibiotic kama vile Amoxicillin, Tetracycline, Clarithromycin au Metronidazole au dawa za kupunguza uzalishaji wa tindikali kwa wingi.

Wagonjwa wengine hutibiwa kwa kufanyiwa upasuaji hasa wale wanaogundulika kuvuja damu ndani ya mwili kupitia vidonda vya tumbo kwani ugonjwa ukifikia hatua hiyo huweza kusababisha kifo iwapo mgonjwa hatapata tiba haraka.

USHAURI
Si vyema na haishauriwi kabisa mgonjwa kujitibu bila kufuata ushauri wa daktari kwani kwa kufanya hivyo anaweza kupata madhara ikiwa atatumia dozi isiyostahili.

MAZIWA YA NG’OMBE HAYAPONYESHII
Ipo dhana kuwa maziwa ya ng’ombe yanaponyesha maradhi haya, ukweli ni kuwa hayaponyeshi vidonda vya tumbo, bali huongeza madhara yatokanayo na ugonjwa huu.

Kitaalamu maziwa huwa na tabia ya kutengeneza aina fulani ya kinga au ukuta (protective coat) kwa vimelea vya Helicobacter Pylori ambayo huvikinga vimelea hivi dhidi ya mashambulizi ya dawa na hivyo kufanya dawa kushindwa kuwaua na kuwaondoa kabisa vimelea hivyo tumboni.


Ukweli ni kwamba maziwa huondoa tu kwa muda maumivu ya tumbo kwa kupunguza makali ya tindikali iliyopo tumboni lakini baadaye maumivu hurejea na kuwa makali.

Wiki ijayo tutaeleza hatu nne za kuugua ugonjwa wa vidonda vya tumbo, usikose nakala yako
imeandaliwa na dr mandai +255 716 300 200
MAKUNDI MATATU YA UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO NA DALILI ZAKE Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com on 12/08/2015 01:37:00 PM Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by habartz © 2014 - 2015
Designed by JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

HABARI NA MATUKIO YA KIJAMIII. Powered by Blogger.