BREAKING NEWS

recent

HILI NDIYO SOKA LA BONGO, AIBU TUPU!

Aibu-3
Soka la Bongo bado litaendelea kusuasua kwasababu moja ya wadau wakubwa wa soka letu bado hawaonekani kujali wala kuthamini kile wanachokifanya kwenye maisha yao ya kila siku ya soka.
Jana ulihcezwa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya JKT Ruvu dhidi ya Castal Union kwenye uwaja wa kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam ambao ulimalizika kwa sare ya kufungana magoli 2-2.
Aibu 1
Kitu ambacho kilishangaza wengi kwenye mchezo huo ni kitendo cha mchezaji wa Coastal Union Nassoro Kapama kuazima ‘vilinda ugoko’ (shin guards) wakati akiingia uwanjani kuchukua nafasi ya Omary Wayne ambaye alikuwa akipumzishwa ili yeye achukue nafasi yake.
Baada ya mwamuzi wa akiba Shafii Mohamed kumgagua kabla hajaingia uwanjani, alibaini mchezaji huyo alikuwa hajavaa vilinda ugo ndipo akamtaka mchezaji huyo kufanya hivyo. Katika hali isio ya kawaida, Kapama alirudi kwenye benchi la Coastal Union lakini hakupata vilinda ugoko hali iliyopelekea kurudi eneo la kufanyia mabadiliko na kusubiri mchezaji anaetoka ili amuombe ampatie vilinda ugoko hivyo.
Aibu 2
Hali hiyo ilizua mawali mwengi kwa mashabiki wa soka ambao walikuwa wanaushuhudia mchezo huo huku baadhi yao wakihoji inakuaje mchezaji anayecheza ngazi ya ligi kuuu tena kwenye klabu kongwe kama Coastal akashindwa kununua vifaa vyake vya michezo kwa ajili ya faida yake yeye mwenyewe.
Aibu
Wachezaji kama hawa wanashusha heshima ya soka la Tanzania kwa kukosa ueledi, kwa hali ya kawaida mchezaji kama Pascal Wawa, Donald Ngoma, Juuko Mursheed au Chidiebele wanaweza kukosa vifaa muhimu kama hivi? Najua jibu litakuwa ni hapana, na hiyo ni kwasababu wanajua kitu wanachokifanya tofauti na wacheaji wengi wa bongo ambao wamekuwa wakiwarudisha nyuma wenzao wanaojaribu kucheza kwenye kiwango cha kimataifa.
HILI NDIYO SOKA LA BONGO, AIBU TUPU! Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com on 12/22/2015 12:11:00 PM Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by habartz © 2014 - 2015
Designed by JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

HABARI NA MATUKIO YA KIJAMIII. Powered by Blogger.