BREAKING NEWZZZZZ; RAIS MAGUFULI ATANGAZA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI
Watanzania wamekuwa na hamu kubwa ya kujua baraza la mawaziri, baada ya kusubira kwa muda mrefu,lakini leo Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli ameamua kutangaza baraza lake la mawaziri.
Katika hatua nyingine Rais Magufuli alisema "Lengo ni kutimiza ahadi yetu ya kuwa na baraza dogo kupunguza gharama na effective kwa kufanya kazi. Zilitengwa bilioni 2, mawaziri watakapoteuliwa waende semina elezi, baraza nitakaloliteua halitakuwa na semina elekezi na fedha tutaelekeza sehemu nyingine kama ni madawati au kwenye elimu bure. Watafanya semina elekezi wenyewe ndani kwa ndani."
WIZARA
Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora: Mawaziri ni George Boniface Taguluvala Simbachawene na Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki, Naibu waziri Selemani Saidi Jafo.
Ofisi ya makamu wa Rais, muungano na mazingira: Waziri ni January Yusuf Makamba, naibu Luhaga Mpina
Ajira, walemavu: Jenista Joakim Mhagama, Naibu nimemtua mbunge, Abdallah Possi. M ambae ni mhadhiri Dodoma
Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu: Waziri ni Jenista Muhagama, manaibu Anthony Mavunde, Possy Abdallah.
Kilimo, mifugo na uvuvi: Waziri ni Mwigulu Lameck Nchemba, naibu William Ole Nasha
Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano: Waziri bado sijamtafuta, naendelea kumfikiria, Naibu waziri mhandisi Edwin Ngonyani.
Fedha na mipango: Waziri bado tunamtafuta, naibu waziri ni Ashantu Kizachi
Nishati na madini: Waziri ni Professa Sospeter M. Muhongo, Naibu waziri ni Medalled Karemaligo
Katiba na sheria: Waziri Harrison George Mwakyembe
Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa: Waziri ni Augustine Philip Mahiga ambae nimemteua kuwa mbunge na kisha waziri, Naibu ni Dr Suzan Kolimba.
Ulinzi na kujenga taifa: Waziri ni Dr. Hussein Ali Mwinyi
Mambo ya ndani: Charles Muhangwa Kitwanga
Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi: Waziri ni William Vangimembe Lukuvi, Naibu Angelina Mabula
Maliasili na Utalii: Waziri bado, naibu ni Ramo Makala
Viwanda, biashara na uwekezaji: Waziri Charles John Poul Mwijage
Elimu,Sayansi Teknolojia na Ufundi: Waziri bado hajapatikana, Naibu ni Stella Manyanya
Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto: Waziri Ummy Ally Mwalimu, Naibu ni Hamisi Andrea Kigwangalla
Habari, utamaduni, wasanii na michezo: Waziri Nape Nnauye, naibu Anastazia Wambura
Wizara ya maji na umwagiliaji: Waziri Makame Mnyaa Mbarawa ambae nilimteua kuwa mbunge, Naibu ni Isack Kamwela
BREAKING NEWZZZZZ; RAIS MAGUFULI ATANGAZA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI
Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com
on
12/10/2015 03:59:00 PM
Rating:
No comments: