UKAWA WAELEZA SABABU ZA WAO KUZOMEA BUNGENI
WABUNGE wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wameelezea sababu zilizowafanya wao kuuchukua uamuzi wa kupiga kelele ndani ya bunge kuwa ni baada ya Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein kuingia Bungeni hali iliyopelekea kutolewa nje ya Bunge hilo.
Mbunge wa jimbo la Hai kwa tiketi ya Chadema ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, Freeman Mbowe alieleza kuwa, walishindwa kuvumilia kuona ujio wa Dk. Shein akiingia Bungeni hapo pamoja na Mh. Pandu Kificho ambaye alidai hivi sasa sio Spika wa Baraza la Wawakilishi kwa kuwa Baraza hilo lilikwisha vunjwa.
Tumeshangaa kuona Pandu Kificho anaingia kama Spika wa Baraza la Wawakilishi wakati Baraza limeshavunjwa, tulishangaa kuona Dk. Shein anaingia kama Rais wa Zanzibar wakati huo kipindi chake cha kukaa madarakani miaka mitano kimekwisha kikatiba, alisema Mbowe.
Naye mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu alisisitiza kuwa wataendelea kuonesha msimamo wao huku akimlalamikia Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai kuwa anaendesha Bunge hilo kibabe
.
“Leo hii askari wenye uniform, mae-FFU askari wa fujo wameingia ndani ya ukumbi wa Bunge. Sasa kwa wasiofahamu, ukumbi wa Bunge katika nchi kama za kwetu na nchi zinazofuata utaratibu kama wa kwetu, Ukumbi wa Bunge huwa haingii mtu yoyote asiyekuwa Mbunge. Ndio maana ili Makamu wa Rais na wale wakubwawakubwa tuliokuwa tunawapigia kelele? waingie, ilibidi tutengue kanuni ili kuwaruhusu waingie”, alisema Tundu Lissu.
Mwenyekiti wa Wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF), Juma Hamad Omary alimtaja Maalim Seif Sharif Hamad kuwa kiongozi anayepaswa kuigwa kwa kuwa aliwahi kukubali kushindwa mara kadhaa licha ya mapungufu kuonekana na kwamba hata alipokuwa Makamu wa Kwanza wa rais na kisha wawakilishi wa CCM kukataa asuhudhurie kwenye sherehe za kufunga Baraza la Wawakilishi, aliamua kutohudhuria.
UKAWA WAELEZA SABABU ZA WAO KUZOMEA BUNGENI
Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com
on
11/22/2015 10:25:00 AM
Rating:
No comments: