BREAKING NEWS

recent

MIAKA MITATU JELA KWA KUKAMATWA NA UBONGO WA BINAADAMU


Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 23 katika jimbo la Indiana Marekani ajikuta mikononi mwa sheria baada ya kukiri kuvunja jumba la makumbusho la afya na kuiba ubongo wa binadamu pamoja na viungo vingine na kuviuza kupitia mtandao

Mwanaume huyo kwa jina la David Charles alikiri mashtaka na atahudumu mwaka mmoja gerezani pamoja na miaka miwili ya majaribio jumla ni mmiaka mitatu

Makumbusho hayo hapo awali ilikuwa hospitali ya watu wenye maradhi ya akili na baadaye ikageuzwa kuwa chumba cha uchunguzi wa maiti na kianatomia.

Makumbusho hyo huhifadhi sampuli za ubongo na viungo vingine vya mwili wa binadamu.

Vitu vingi alivyokuwa anauza mwanaume huyo vilitambulika baada ya mtu mmoja kutoka San Diego kufanya uchunguzi kupitia mtandao na kugundua kuwa vilikuwa ni vya uwizi.

Aidha wapelelezi walimpata Charles kwa urahisi kwani alikuwa amesahau kipande cha karatasi chenye alama za vidole vyake vilivyokuwa na damu katika jumba hilo la makumbusho.

trt swahili.
MIAKA MITATU JELA KWA KUKAMATWA NA UBONGO WA BINAADAMU Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com on 11/26/2015 03:54:00 PM Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by habartz © 2014 - 2015
Designed by JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

HABARI NA MATUKIO YA KIJAMIII. Powered by Blogger.