BREAKING NEWS

recent

MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUINGIA KWENYE MAHUSIANO

Sina Tafsiri nzuri kuhusu mahusiano ya kimapenzi, tunatofautiana sana inapokuja swala la nini unataka mpenzi wako awenacho na vigezo vipi vinakuvutia kama ni kazi yake nzuri mvuto wake ama gari yake nzuri.

Hakikisha vigezo vyako ni sahihi kwani unapoingia katika mahusiano si wakati wote inakuwa rahisi kutoka, wapo wanawake wanao umizwa na kuvumilia hapo walipo sababu tu wanaamini watawabadilisha hao wapenzi wao hasa watakapofunga ndoa. Hao wanaitwa Mr. Wrong huwezi mbadili Mr. Wrong hiyo ni Full time job.
Usipoteze muda na wanaume wa aina hiyo, je unajua unataka nini katika mahusiano? Yapo mambo machache ya kuzingatia kabla hujajiachia mzima mzima katika dimbwi la mahusiano


                                                                SIO MSIKIVU:
Wanawake wote wanaelewa ni kiasi gani inakera kuwa na mwanaume asiye msikivu, wanawake tunapenda kuwashirikisha matatizo yetu wapenzi wetu huwa tunataka mwanaume anae sikiliza na sio anaetaka kutatua matatizo kwajiri yetu.
Mwanaume anaesikiliza ni rahisi kutatua matatizo pamoja
Matatizo huanza katika mahusiano kama hakuna mawasiliano ya karibu na usikivu na hapo ndipo shida huanza.
                                                  ASIYE NA ADABU (HESHIMA):
Kama umetoka na mpenzi wako mara kadhaa na ukaona akiongea na muhudumu wa magahawa ama Yule mlinzi wa getini kwa lugha chafu na dharau achana nae kimbia
Kama anashindwa kuwaheshimu watu sababu tu anawaona wako chini sana kwake hawezi kukuheshimu wewe pia,
Njia nyingine ya kujua si mwenye adabu chunguza anavyoongea na mama ake, kama hana adabu wala heshima kwa mamaake mzazi my Dear, we utakuwa nani kwake mpaka upate heshima zote amka huyo si mwanaume.
Heshima ni kupeana nafasi hamuwezi kufanana kila kitu hasa inapokuja swala la vitu mpendavyo (interests) ila ni jinsi gani mnakabiliana na tofauti zetu hilo ndio muhimu
Kukuacha uangalie tamthilia mara moja moja hata km yeye havutiwi akuruhusu kutoka na marafiki zako hata mara moja moja.
Ndani ya wiki 2 au 3 katika mahusiano unaweza jua kama mwanaume ana heshima au hana.

                                                    KUKUTHAMINI:
Wanawake tunapenda vitu vidogo vidogo sana katika mapenzi sio lazima ufanye makubwa yasiyo elezeka kuonyesha unajali, lakini si lazima kila siku ukutane na mpenzi wako mikono mitupu beba hata chocolate, ice cream, maua si mbaya mara moja moja. kumbuka siku yake ya kuzaliwa na ufanye ajisikie wa kipekee kila unapokuwa karibu yake.

                                                            MKOROFI:
Mkimbie mwanaume mkorofi , mwepesi wa kunyanyua mkono wake na kukupiga, ogopa mwanaume anaetaka kukufwata kila kona hayo sio mapenzi kimbia. Mwanaume wa aina hiyo anahitaji daktari sio mpenzi sababu sio mzima, wanaitwa “stalkers” hawa ni zaidi ya wapelelezi kuwa mbali na mtu wa aina hii.

                                                               GUBU:
Kuna wale wanaongea sana, hakuna zuri kwake kila unachofanya kwake ni maneno tu analalamika vitu visivyo na maana asubuhi mchana usiku, akipiga simu hakuna salamu ni malalamiko tuu, mtu kama huyu ukiwa nae ndani ni zaidi ya Mama makwe, huwa hawaridhiki kwa lolote sio chakula wala mapenzi umpatiayo ukiona ishara hizi kimbia
MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUINGIA KWENYE MAHUSIANO Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com on 10/09/2015 02:29:00 PM Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by habartz © 2014 - 2015
Designed by JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

HABARI NA MATUKIO YA KIJAMIII. Powered by Blogger.