BREAKING NEWS

recent

UTAFITI WA TWAWEZA WAIBEBA CCM.....KAMA UCHAGUZI UNGEFANYIKA LEO ASILIMIA 65% WALISEMA MAGUFULI, 25% WALISEMA LOWASSA.




Taasisi ya Twaweza imetoa utafiti wake ambao inasema imefanya kwa wananchi wa Tanzania bara kutoka mikoa tofauti ya Tanzania.

Swali la kama uchaguzi ungefanyika leo, ungempigia kura mgombea wa chama gani? wanasema watu wamejibu kama ifuatavyo
CCM - 66%
CHADEMA - 22%
CUF - 1%
ACT wazalendo - 0%
UKAWA - 3%
Kingine - 6%
Hakuna jibu 2%

Utafiti huo uliotokana na kuhoji watu 1848 kutoka mikoa tofauti ya Tanzania bara, inasema iliwauliza wananchi hao: Ukimwacha Rais Kikwete, iwapo uchaguzi wa urais ungefanyika leo, ungemchagua nani?

...Majibu ya swali hilo TWAWEZA wanasema limejibiwa na wananchi hao kama ifuatavyo

Magufuli 65 %
Lowassa 25%
Mwingine 3%
Sijui/kataa jibu 7%

Akitangaza utafiti huo leo, Mkurugenzi mtendaji wa TWAWEZA, Aidan Eiyakuze amesema kwa upande wa ubunge, Utafiti huo unaonyesha kuwa CCM inaongeza kwa asilimia 60 na kufuatiwa na CHADEMA asilimia 26.
UTAFITI WA TWAWEZA WAIBEBA CCM.....KAMA UCHAGUZI UNGEFANYIKA LEO ASILIMIA 65% WALISEMA MAGUFULI, 25% WALISEMA LOWASSA. Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com on 9/23/2015 07:49:00 AM Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by habartz © 2014 - 2015
Designed by JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

HABARI NA MATUKIO YA KIJAMIII. Powered by Blogger.