BREAKING NEWS

recent

TANZANIA ITAENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU.


                                                          Mh Jakaya M Kikwete

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dakta Jakaya Kikwete amesema Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa mahakama ya Afrika ya haki za binadamu yenye makao yake jijini Arusha ili kuhakikisha kuwa inafikia malengo ya uanzishwaji wake wa kusimamia haki kwa waafrika. 

Rais Dakta Kikwete anatoa kauli hiyo jijini Arusha alipokutana na wafanyakazi wa mahakama hiyo na kuzindua taarifa za msingi za mahakama zilizotafsiriwa kwa lugha ya kiswahili ambapo anaongeza kuwa serikali yake kama mwenyeji wa mahakama tayari imetoa eneo la ekari ishirini katika eneo la lakilaki wilayani Arumeru kwa ajili ya ujenzi wa makao yake ya kudumu.

Akizungumzia umuhimu wa taarifa hizo kuwekwa kwatika lugha ya kiswahili, rais wa mahakama hiyo ya Afrika ya haki za binadamu jaji Agustino anasema itaongeza uelewa kwa nchi zinazozungumza kiswahili na kupanua wigo wa kuitumia mahakama hiyo kupata haki.

Mahakama ya Afrika ya haki za binadamu iliyoanza shughuli zake rasmi Novemba 2006 baada ya itifaki ya uanzishwaji wake kukubaliwa nchini Burkina Faso mwaka 1998 ilianzishwa na nchi wanachama wa umoja wa Afrika kwa lengo la kuimarisha haki za binadamu na watu barani Afrika na kuimarisha jukumu tume ya Afrika ya haki za binadamu na watu maarufu kama tume ya Banjul.
TANZANIA ITAENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU. Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com on 9/12/2015 08:00:00 AM Rating: 5
All Rights Reserved by habartz © 2014 - 2015
Designed by JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

HABARI NA MATUKIO YA KIJAMIII. Powered by Blogger.