BREAKING NEWS

recent

RAIS KIKWETE ASEMA NCHI ZA AFRIKA HAZITAWEZA KUZUNGUMZIA MAENDELEO BILA KUBORESHA MIUNDOMBINU.

Rais Jakaya Kikwete amesema nchi za Afrika hazitaweza kuzungumzia mipango ya maendeleo bila ya kuboresha miundombinu na mifumo itakayowezesha upatikanaji na matumizi sahihi ya takwimu kwa ajili ya maendeleo.

Akifungua mkutano wa kwanza wa kimataifa wa takwimu huria kufanyika Afrika uliohudhuriwa na nchi zaidi 30, rais Kikwete amesema takwimu ni nyenzo muhimu ya maendeleo na hakuna mafanikio yanayoweza kupatikana bila ya matumizi ya takwimu sahihi kwa vile zinazewezesha kutambua changamoto za kijamii na kiuchumi na kusisitiza moja ya changamoto za nchi za Afrika ni upatikanaji wa takwimu sahihi.

Awali waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mhe. Mathias Chikawe amesema katika ulimwengu wa digitali takwimu huria imekuwa moja na nyezo muhimu katika kuimarisha uwazi na uwajibikaji na kupeleka huduma kwa jamii ikiwa ni pamoja na kuendeleza ubunifu ambapo amesema moja na malengo ya mkutano huo ni kubadilishana uzoefu na wadau kutoka nchi mbalimbali wakiwemo asasi za kirai, serikali na sekta binafsi. 

Aidha akizungumza na waandishi wa habari, katibu mkuu kiongozi balozi Ombeni Sefue amesema mfumo wa takwimu huria unawezesha upatikanaji wa takwimu za serikali kwa uwazi ambapo Tanzania imeanza na wizara ya afya, maji na elimu kwa kuwa zinagusa jamii moja kwa moja na kusisitiza mpitia mfumo huo wananchi wanaweza kuihoji serikali na kuiwajibisha.
RAIS KIKWETE ASEMA NCHI ZA AFRIKA HAZITAWEZA KUZUNGUMZIA MAENDELEO BILA KUBORESHA MIUNDOMBINU. Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com on 9/05/2015 09:32:00 AM Rating: 5
All Rights Reserved by habartz © 2014 - 2015
Designed by JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

HABARI NA MATUKIO YA KIJAMIII. Powered by Blogger.