MGOMBEA MWENZA WA UKAWA AAHIDI NEEMA KWA WAKAZI WA KIGAMBONI.
Kampeni za uchaguzi mkuu zimeendelea kwa kishindo katika jiji la Dar es Salaam, ambako mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA ), kupitia umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA )Mh. Juma Duni Haji amewataka wananchi wa jimbo la Kigamboni kumchagua Mh. Edward Lowassa ambaye tangu akiwa waziri mkuu ameonyesha dhamira ya kweli ya kuuchukia umaskini, huku akipania kuboresha maisha ya wajasiriamali wakiwemo waendesha pikipiki za bodaboda na mama lishe.
Baada ya kuwasili katika eneo la kigamboni kwa kutumia usafiri wa kivuko, mgombea mwenza wa urais wa chadema Mh.Juma Duni Haji ambaye alifuatana na mwenyekiti mwenza wa UKAWA Mh. James Francis Mbatia,moja kwa moja akaelekea katika viwanja vya tungi kuwahutubia maelfu ya wananchi wa mji wa kigamboni na viunga vyake waliokuwa wakimsubiri kwa shauku kubwa ili kusikiliza sera za UKAWA kuhusu mustakabali wa maisha yao.
Mwenyekiti wa chama cha NCCR – Mageuzi Mh.James Mbatia akasema ili kuwa na mji mpya wa kisasa wa kigamboni amebainisha malengo 17 endelevu ya dunia ambayo yatasainiwa makao makuu ya umoja wa mataifa NEW YORK, Marekani Septemba mwaka huu- amesema wakazi wa kigamboni wanapaswa kushirikishwa katika mpango wa matumizi bora ya ardhi katika hatua zote ili kufahamu watapata asilimia ngapi katika uwekezaji huo.
Mh.Mbatia ambaye pia ni mgombea ubunge wa jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro amezungumzia suala la nauli ya shilingi 200 wanayolipa watumiaji wa kivuko hicho
MGOMBEA MWENZA WA UKAWA AAHIDI NEEMA KWA WAKAZI WA KIGAMBONI.
Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com
on
9/21/2015 03:06:00 PM
Rating:
No comments: