BREAKING NEWS

recent

MASHAMBA YA WAWEKEZAJI YASIYOENDELEZWA KUPEWA WANANCHI UKAWA IKIINGIA MADARAKAN


Mgombea mwenza wa urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Demokrasia na maendeleo( CHADEMA ),chini ya mwavuli wa vyama vinavounda umoja wa katiba ya wananchi( UKAWA )Mh.Juma Haji Duni ameendelea kunadi sera za chama hicho na kumuombea kura mgombea wake wa urais Mh. Edward Lowassa kwa wananchi wa mkoa wa Iringa,ambapo amewahaidi wakazi wa jimbo la Isimani na Kalenga kwamba wakiingia madarakani watarejeshewa mashamba yao ambayo serikali ya chama cha mapinduzi iliyabinafsisha kwa wawekezaji lakini matokeo yake wameshindwa kuyaendeleza.

Akihutubia mikutano ya kampeni za uchaguzi mkuu katika majimbo ya Isimani na Kalenga baada ya kumaliza mchakamchaka wa kampeni hizo katika majimbo ya mikoa ya Kusini ya Lindi na Mtwara pamoja mikoa ya Pwani,Tanga na Dar es Salaam Mh.Duni amesema kuwa iwapo watanzania watamchagua Mh.Lowassa,atahakikisha wakulima na wafugaji wanaingizwa katika mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kumaliza migogoro sanjari na kuwajengea mazingira mazuri wafanyabiashara ndogondogo kwa kuwaondolea utitiri wa kodi ambazo zinadaiwa kuwanufaisha baadhi ya watu wachache.

Patrick Ole Sosopi ni mgombea ubunge wa jimbo la isimani kupitia Chadema ambaye anasema akichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha maisha ya wananchi wanaoishi jirani na hifadhi ya taifa ya ruaha yanakuwa ya amani na furaha badala ya kuwa ya mateso na majuto kutokana na operesheni tokomeza ambayo amedai mpaka sasa inaendelea.

Hatimaye ikafika zamu ya makada wa vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi kupanda jukwaani kwa nyakati tofauti ili kuwaelezea wananchi ni mambo gani ambayo endapo Mh.Edward Lowassa atapata ridhaa ya kuwa rais wa serikali ya awamu ya tano atayafanya.

MASHAMBA YA WAWEKEZAJI YASIYOENDELEZWA KUPEWA WANANCHI UKAWA IKIINGIA MADARAKAN Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com on 9/11/2015 04:15:00 PM Rating: 5
All Rights Reserved by habartz © 2014 - 2015
Designed by JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

HABARI NA MATUKIO YA KIJAMIII. Powered by Blogger.