BREAKING NEWS

recent

CHAMA CHA NCCR MAGEUZI KIMEWATAKA WATANZANIA KUCHAGUA VIONGOZI BORA


Chama cha NCCR mageuzi kimezindua kampeni zake katika jimbo la vunjo mkoani Kilimanjaro na kuwataka watanzania kuchagua viongozi wenye sifa watakaoweza kusimamia raslimali zilizopo hapa nchini ili ziwanufaishe wananchi kuondokana na umaskini na kuepusha taifa kutegemea fedha za wahisani kusaidia bajeti ya nchi.

Mwenyekiti wa chama cha NCCR mageuzi ambaye pia ni mgombea ubunge wa jimbo la Vunjo Mh.James Mbatia amesema Tanzania ni nchi tajiri sana ambayo ina uwezeo wa kujiendesha yenyewe bila kutegemea fedha za wahisani endapo raslimali zilziopo hapa nchini zitasimamiwa vizuri.

Amesema amefanya utafiti na kubaini fedha ambazo zimetumiwa na viongozi katika safari za kwenda nje ya nchi kwa kipindi cha miaka 10 zimegharimu zaidi ya shilingi trilioni 10 na kwamba endapo fedha hizo zingetumika vizuri zingeweza kujenga hospitali za rufaa katika wilaya zote hapa nchini.

Amesema endapo watanzania watampa mgomea urais wa vyama vinavyunda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA Mh.Edward Lowassa ridhaa ya kuiongoza Tanzania watahakikisha wanaleta mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kulipa madeni yote ya walimu na kuondoa kodi inayokatwa kwenye mishahara ya wafanyazi.

Kwa upande wake mbunge wa bunge la jumuiya ya Afrika Bashariki Bi Nderakindo Kessy amesema umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) ndiyo njia pekee ya kuleta demokrasia ya kweli hapa nchini na kuondoa mipaka iliyowekwa na wakoloni katika nchi za Afrika.

Mjumbe wa halimashauri kuu ya chama cha NCCR mageuzi taifa Hemed Msabaha na mkurugenzi wa uchumi na fedha kutoka chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Bw.Antony Komu wamesema miaka 50 ya uhuru bado taifa linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mzigo mkubwa wa deni la zaidi ya shilingi tlirilioni 35.
CHAMA CHA NCCR MAGEUZI KIMEWATAKA WATANZANIA KUCHAGUA VIONGOZI BORA Reviewed by habarinamatukioyakijamii.brogspot.com on 9/06/2015 02:02:00 PM Rating: 5
All Rights Reserved by habartz © 2014 - 2015
Designed by JOJOThemes

Contact Form

Name

Email *

Message *

HABARI NA MATUKIO YA KIJAMIII. Powered by Blogger.